Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akipeana
mkono na Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing, walipokutana
katika viwanja vya Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba),
Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akitoa maelekezo
kwa wafanyakazi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuhusu namna ya
kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kukata bima ili
kujikinga na majanga, alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha na Mipango
lilipo katika viwanja vya maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara
(sabasaba), Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika hilo Bw. Sam Kamanga.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia)
akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa uendeshaji wa Wakala wa Huduma ya
Ununuzi Serikalini (GPSA), Naftal Sigwejo baada ya kuulizwa kuhusu ubora
wa baadhi ya bidhaa zinazotolewa Serikalini baada ya kutembelea Banda
la Wizara ya Fedha na Mipango katika Maonesho ya 41 ya Biashara ya
Kimataifa (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia)
akimpongeza Mzazi wa kijana Msuya Mageta (katikati) aliyejiunga na Mfuko
wa Pensheni wa PPF kupitia mpango wa Wote Scheme katika Banda la Wizara
ya Fedha na Mipango kwenye Maonesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara
(Sabasaba), Jijini Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...