Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesimamisha umiliki wa mwekezaji wa mashamba ya katani yanayomilikiwa na kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited yaliyopo kata ya Mnazi wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Waziri Lukuvi amefikia uamuzi huo baada ya wakazi wa eneo hilo kuzuia msafara wake na kupata malalamiko mengi kutoka kwa wananchi hao na viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Lushoto wakimlalamikia Waziri kuhusu mashamba matatu ya Mnazi yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo bila kuendelezwa na kusababisha migogoro kwa awakazi wa Mnazi.

Baada ya kupokea malalamiko hao Waziri Lukuvi aliamua kutembelea mashamba hayo na kuyakagua ili kujionea hali halisi na kuwasikiliza wananchi ambao wamekuwa wanakabiliwa na mgogoro huu kwa miaka mingi.

Baada ya kutembelea na kujiridhisha Waziri Lukuvi amesema kwamba shamba hilo linastahili kufutwa kama ilivyopendekezwa na ofisi ya Mkoa wa Tanga na ofisi ya Kamishna wa Ardhi Kanda ya Kaskazini kwa kuwa mmiliki ameshindwa kuwa na sifa za umiliki kwa kuwa hajalipa kodi ya ardhi tangu mwaka 2004, hajalipa wafanyakazi wake kwa muda mrefu, miundombinu yake na mazingira ya kazi hayaridhishi na ameshindwa kuliendeleza shamba hilo tangu akabidhiwe mwaka 1997 kwa kurithi mashine na mitambo ileile ya mkoloni ya mwaka 1937.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wakazi wa kata ya Mnazi wilaya ya Lushoto mkoni Tanga waliozuia msafara wake na kumpa malalamiko kuhusu mashamba matatu yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo bila kuendelezwa na kusababisha migogoro.  
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikagua miundombinu na mazingira ya kazi ya mwekezaji wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ambaye ameshindwa kuindeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997. 
Mazingira ya shamba yaliyotelekezwa na mmiliki wake wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ambaye ameshindwa kuindeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997. 
Baadhi ya mitambo iliyochakaa ambayo mwekezaji wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ameshindwa kuiendeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997 kwa kurithi mashine na mitambo hiyo kutoka kwa mkoloni tangu mwaka 1937. 
Baadhi ya mitambo iliyochakaa ambayo mwekezaji wa kampuni ya Le-Mash Enterprises Limited ameshindwa kuiendeleza tangu akabidhiwe mwaka 1997 kwa kurithi mashine na mitambo hiyo kutoka kwa mkoloni tangu mwaka 1937.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...