Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi awasili mkoani Tanga kutatua migogoro ya ardhi inayoukabili mkoa huo pamoja na mikoa inayopakana nayo.
Katika ziara hii Waziri Lukuvi leo amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera ili kutatua migogoro ya mipaka iliopo kati ya Wilaya ya Kiteto Iliyopo Mkoani Manyara na Wilaya ya Kilindi iliyopo mkoani Tanga ikiwa muendeleo zo wa mikutano ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro huu ambao umesababisha uvunjifu wa amani.
Waziri Lukuvi anatekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe. Khassim Majaliwa ambae alimuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kutatua mgogoro huu uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo mbili pindi alipofanya ziara yake mkoani Tanga.

Ikumbukwe mnamo tarehe 18 Januari, 2017 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya  ziara Wilayani Kilindi katika Kijiji cha Mafisa na kuzungumza na wanachi Kijijini hapo kuhusiana na mgogoro huo na kutoa maagizo kwa viongozi wa kuchaguliwa kuacha kutumia nafasi zao vibaya kuongoza kwa mihemko au ushabiki kwa kuwa kufanya hivyo kunapelekea wananchi kufuata ushabiki na kuvunja sheria zilizopo.
Ili kutekeleza agizo hili wakuu wa mikoa hii miwili wakiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wamekutana ikiwa ni muendelezo wa vikao vya kulitafutia ufumbuzi suala hili.
Aidha, wawakilishi wa wakazi wa kata ya Mnazi wilayani Lushoto na viongozi wa Halmashauri ya Lushoto walimlalamikia Waziri Lukuvi kuhusu mashamba matatu ya Mnazi yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo ajulikanae kwa jina la Le-Mash Enterprises Limited.
Baada ya Waziri Lukuvi kusikiliza malalamiko hayo, ameahidi kutembelea mashamba hayo kesho ili kujionea hali halisi na kuwasikiliza wananchi ambao wanakabiliwa na mgogoro huu ambao umekuwepo kwa miaka mingi.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera wakiwasikiliza wataalamu kutoka Wizara ya Ardhi katika kutatua mgogoro wa mpaka unaoikabili mikoa hiyo.
 Wawakilishi wa wakazi wa kata ya Mnazi wilayani Lushoto na viongozi wa Halmashauri ya Lushoto wakiwasilisha malalamiko yao kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi baada ya kukutana nae.
 Eneo la Mji wa Lushoto mkoani Tanga.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi  (katikati) alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela (wanne kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera na (watatu kushoto) pamoja na viongozi wengine.
 Wawakilishi wa wakazi wa kata ya Mnazi wilayani Lushoto na viongozi wa Halmashauri ya Lushoto wakiongozwa na Mbunge wa Mlalo Mhe. Rashid Shangazi (wasita Kulia) walipokutana Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...