WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Shirika la Nyumba (NHC) kwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mnolela mkoani Lindi kwa muda mfupi. 
Amesema ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa ulianza mwezi Machi 2017 na sasa tayari  umekamilika, jambo ambalo litarahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo na wa jirani. 
Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo Alhamisi, Julai 13, 2017 alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Mnolela baada ya kuzindua zahanati hiyo iliyosimamiwa na NHC. Alisema ujenzi wa zahanati hiyo ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha huduma za afya kwa kusogeza huduma karibu kwa wananchi wake. 
“Rais wetu Dkt. John Magufuli amedhamiria kuwaondolea wananchi changamoto za mbalimbali zikiwemo za huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.” 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa NHC, Bw. Nehemia Mchechu alisema mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo ulisimamiwa na NHC na umegharimu sh. milioni 65.5. 
“Shilingi milioni 15 zilitolewa na Rais. Dkt. Magufuli, sh. milioni 10 zilitolewa na Mheshimiwa Mbunge wa jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye, NHC ilitoa sh. milioni 10 na kiasi kilichosalia ni mchango wa halmashauri.” 
Awali Mbunge wa jimbo la Mtama, Mheshimiwa Nape alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa mchango mkubwa alioutoa katika mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo. 
Mheshimiwa Nape alisema zahanati hiyo ni mkombozi kwa wakati wa kijiji cha Mnolela na wananchi wengine wanaoishi kwenye maeneo yaliyo jirani na kijiji hicho.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC),wakati alipofungua Zahanati katika kijiji cha Mnolela, akiwa  njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (katikati) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye Julai 13, 2017.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akikata utepe wakati alipofungua Zahanati katika kijiji cha Mnolela, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne (kutoka kushoto) ni Mbunge wa  Jimbo la Mtama Nape Mnauye, Diwani Kata ya Mnolela Omar Liveta, Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC) kutoka kulia ni Meneja NHC Lindi Gibson Mwaigomole, Meneja NHC Mtwara Nehemia Msigwa, Mkuu wa Mkoa Lindi Godrey Zambi Julai 13, 2017.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akikagua wakati kifaa katika Zahanati ya Mnolela, baada ya kuifungua, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,akizungumza na wananchi wa Mnolela mara baada ya kuifungua Zahanati hiyo iliyopo katika Kijiji cha Mnolela, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...