WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania wanaofanya kazi katika viwanda mbalimbali nchini kufanya kazi kwa bidii na kuwa waaminifu. 
Amesema Tanzania imedhamiria kukuza uchumi wake kupitia sekta ya viwanda hivyo ni vema watakaopata fursa ya ajira katika viwanda hivyo kuwa waadilifu.
Ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 30, 2017) wakati akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha gesi cha Ikama kilichoko wilayani Rungwe. Waziri Mkuu amesema wakati Serikali ikiendelea kuwakaribisha wawekezaji nchini, wananchi walioajiriwa kwenye maeneo hayo wawe waaminifu.
“Mnatakiwa muwe waaminifu, msibebe kitu chochote ndani ya kiwanda bila ya ridhaa ya wamiliki kwa kuwa mtaonyesha taswira mbaya kwa wawekezaji.” Amesema uaminifu wao ndio utawezesha Watanzania wengi kupata ajira kwenye viwanda hivyo ambavyo vimejengwa katika maeneo yao.
Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na kampuni ya TOL Gases, Mhandisi Harold Temu alisema kiwanda kinauwezo wa kuzalisha tani 46 kwa siku. Alisema gesi inayozalishwa kiwandani hapo ni ya Carbon Dioxide ambayo inauzwa nchini na nchi jirani za Zambia, Malawi, Zimbabwe na Congo.
Mhandisi Temu alisema wateja wakubwa wa gesi hiyo ni viwanda vya kutengenezea soda, bia na pia hutumika katika kuhifadhia chakula na kwenye vifaa vya kuzimia moto. Mapema Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kuchakata majani ya chai cha Katumba, ambapo alisema Serikali inaimarisha Ushirika wa zao hili ili wakulima waweze kupata tija. 

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma wa wilaya ya Rungwe Julai 30, 2017. Kulia ni Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla. 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha chai cha Katumba wilayani Rungwe Julai 30, 2017. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla na kushoto ni Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Bw. Ramadhani Kampasili. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akitazama chai iliyosindikwa na kufungashwa tayari kwa kuuzwa wakati alipotembelea kwianda cha chai cha Katumba wilayani Rungwe Julai 30, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ufundi, Bw. McJohn Mbiri (kulia Kwake) kuhusu mitambo ya kuzaisha gesi ya hewa ya ukaa wakati alipotembelea kiwanda cha TOL Limited kilichopo katika kijiji cha Ikama wilayani Rungwe Julai 30, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,  Mhe. Amos Makalla. 
Sehemu ya watumishi wa umma wa wilaya ya Rungwe wakimsikiliza Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alipozungumza nao leo Julai 30, 2017. 

(Picha na Ofisi ya Waziri ) 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...