WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempa miezi miwili kuanzia leo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Songwe, Bw. Elias Nawera abadili mwenendo wake kiutendaji na ashirikiane vizuri na  Mkuu wa wilaya hiyo Bw. Samwel Jeremiah.
Amesema Serikali ya awamu ya Tano inawataka watumishi wote kufanya kazi kwa ushirikiano na kuheshimiana na atakayeshindwa kufanya hivyo hatavumiliwa.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Julai 20, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Songwe akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Songwe.
Amesema watumishi wote wanatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi yaweze kufikiwa. Pia waheshimiane sehemu za kazi na kila mtu azingatie mipaka ya madaraka yake.
"Mkurugenzi hapa hamsikilizi Mkuu wa wilaya anaondoka kituo cha kazi bila ya kuaga na amewagawa wakuu wa Idara. Namtaka afanye mabadiliko ya utendaji wake ndani ya miezi miwili na Mkuu wa Mkoa fuatilia jambo hili."
Pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya wote wasimamie utendaji wa wakurugenzi wa Halmashauri kwenye maeneo yao ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo.”Serikali hii si ya mchezo. Serikali hii inahitaji watumishi waadilifu wa kuwatumikia Watanzania.”
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Bibi Chiku Galawa amesema wamejipanga kuhakikisha changamoto zote zinazoukabili mkoa zinaboreshwa pamoja na kufikia malengo ifikapo 2020.
Ametaja malengo hayo kuwa ni kuhakikisha mkoa huo unakuwa kinara katika ukusanyaji wa mapato, kila mwananchi awe na bima ya afya pamoja na kuwa na hospitali katika kila wilaya.
Kuhusu mpango wa Serikali wa kuwa na uchumi wa viwanda amesema tayari wameshaanzisha viwanda vya maziwa, kukamua alizeti ikiwa ni kuunga mkono mpango huo.
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa baada ya kuwasili Mkwajuni wilayani Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Songwe Julai 20, 2017. Kulia ni mkewe Mary.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Songwe, Elias Nawela  baada ya kuwasili Mkwajuni wilayani Songwe kuanza ziara ya mkoa wa Songwe Julai 20, 2017. Kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa. 
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimia wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  (kulia) alipozungumza na watumishi wa umma na viongozi wa dini  kwenye ukumbi wa Chuo cha Uuguzi cha  Kanisa Katoliki cha Mwambani wilayani Songwe, Julai 20, 20117. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.  
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma na viongozi wa dini wa mkoa wa Songwe kwenye ukumbi wa Chuo cha Uuguzi cha Kanisa Katoliki cha Mwambani wilayani Songwe, Julai 20, 2017. Kushoto ni Mkewe Mary na Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...