*Asema watu wengi wamekufa wakikatiza katika eneo hilo
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa daraja la mto Lukuledi lenye urefu wa kilomita 30.45 linalounganisha mikoa ya Lindi na Mtwara na na kusema kwamba ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wake.
Amesema ujenzi wa daraja hilo unatakaogharimu sh. bilioni 5.4 ni mkombozi kwa wananchi wa mikoa hiyo hasa wa wilaya za Ruangwa na Masasi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakishirikiana katika masuala mbalimbali yakiwemo kilimo na huduma za kijamii. 
Waziri Mkuu amesema hayo leo Jumanne, Julai 11, 2017  alipotembelea mradi huo wa ujenzi wa daraja hilo katika kijiji cha Nandanga alipowasili wilayani Ruangwa akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi.
“Watu wengi wamepoteza maisha kwa kuliwa na mamba walipokuwa wakikatiza katika eneo hilo. Ujenzi wa daraja hili ni muhimu, watu wengi wa Ruangwa wanavuka kufuata matibabu katika hospitali ya Ndanda, wilayani Masasi na wakazi wa Ndanda wanavuka kufanya shughuli za kilimo wilayani Ruangwa.”
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo ya mradi wa daraja la Nandaga, linalo unganisha Wilaya ya Ruangwa na Wilaya ya Masasi, kutoka kwa Mhandisi Josam Mlaki, kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) . 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua mradi wa daraja la Nandaga, linalo unganisha Wilaya ya Ruangwa na Wilaya ya Masasi, kutoka kwa Mhandisi Josam Mlaki, kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...