*Ni baada ya kulisababishia Jiji la Mbeya hasara ya sh. bilioni 63

WAZIRI Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Mbeya Bw. Emanuel Kiabo kumkamata na kumuhoji Mhe. Athanas Kapunga aliyekuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya na wenzake 11 kwa tuhuma za kuisababishia Serikali hasara ya sh. bilioni 63.448.
"Serikali hii haiwezi ikawaacha watu hawa ambao wameisababishia hasara kubwa kiasi hiki tena kwa halmashauri moja. Kama wako humu ndani naagiza wakamatwe na waanze kuhojiwa na ambao wamestaafu au kuhamishwa kituo cha kazi wasakwe popote walipo ili nao waje kuhojiwa.”

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo Jumatatu, Julai 31, 2017 alipozungumza na watumishi wa Halmashauri za wilaya ya Mbeya na Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Benjamin Mkapa.

Wengine ni waliowahi kuwa wakurugenzi wa Jiji hilo ambao ni Bw. Mussa Zungiza, Bi. Elizabeth Munuo, Bw. Juma Idd na Dkt. Samwel Lazaro aliyekuwa akikaimu nafasi ya Ukurugenzi.

Wengine ni aliyekuwa Mweka Hazina wa Jiji, Bw. James Jorojik pamoja na waliokuwa wajumbe wa Bodi ya Zabuni ambao ni Bw. Mussa Mapunda, Bw. Samweli Bubengwa, Bw. Davis Mbembela, Bi. Lydia Herbert na Bw. Bernard Nsolo ambao wanatuhumiwa kwamba walipitisha nyongeza ya mradi huo bila ya kuzingatia maslahi ya Jiji pamoja Emily Maganga ambaye hakuishauri vizuri bodi hiyo.

Waziri Mkuu amesema watumishi hao wanatakiwa kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria kwa kuwa wameisbabishia Serikali harasa kubwa katika mradi wa ujenzi wa soko la Mwanjelwa Jijini Mbeya ambalo hadi sasa halijaonyesha tija.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa TAKUKURU wa Mkoa wa Mbeya, Mhandisi Emmanuel Kyabo taarifa zinaoonyesha ubadhirifu uliofanywa na baadhi ya watendaji katika ujenzi wa soko la Mwanjelwa jijini Mbeya ili afanye uchunguzi wa kina  na kumshauri Waziri Mkuu hatua zinazostahili kuchukuliwa kwa watakaobainika kuwa wamefanya makosa. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafisi wa Manispaa ya Mbeya kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya Julai 31, 2017.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla na Kulia ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson. 
 Baadhi ya Watumishi wa Umma, Viongozi wa Dini na Viongozi wa Taasisi Binafsi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Benjamin Mkapa jijini Mbeya julai 31, 2017. 
Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...