Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam 

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kuamuru kituo cha Mafuta cha GBP kifungwe hadi hapo kitakapo funga mashine maalumu za kutolea risiti baada ya kubainika hakitumii ipasanyo mashine za kieletroniki za kukusanyia kodi (EFD) 

Dkt. Mpango amechukua hatua hiyo baada ya kujionea kituo hicho kikiwa na  pampu nne za mafuta lakini kuna mashine moja pekee ya mkononi ya kutolea  risiti jambo linasababisha wateja wao wengi kutopewa risiti na hivyo kuikosesha Serikali mapato yake na ni kinyume cha sheria za nchi. 

“Sasa nawachukulia hatua ili liwe fundisho kwa wengine wote wanaouza mafuta nchini bila kufuata taratibu, na nitaanza na wewe, biashara yako isimame mpaka mashine zifungwe kwenye kituo chote na utekeleze mara moja” alisistiza Dkt. Mpango 

Katika ukaguzi wa Kituo cha Mafuta cha Puma, Dkt. Mpango amesifu utaratibu mzuri uliowekwa na kituo hicho kwa kufunga mashine maalumu za kutolea risiti zilizounganishwa na kila pampu za mafuta kitu ambacho ndicho Serikali inavitaka vituo vyote vya mafuta vitumie mfumo huo 

“Kituo hiki kimezingatia sheria sheria kwa kufunga mashine kwa kuzingatia maelekezo ya Serikali na hapa tunauhakika wa kupata fedha za kuwatumikia wananchi, kinyume kabisa na kituo cha mafuta nilichokifungia, hapa ndio ningeomba Watanzania wanunue mafuta” aliongeza Dkt. Mpango. 




Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (aliyevaa tai) akimhoji mmoja wa wahudumu wa Kituo cha mafuta cha GBP kilichopo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kabla ya kukifunga kwa kosa la kutotumia Mashine za kierektroniki za EFDs. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akitoa agizo kwa msimamizi wa Kituo cha Mafuta cha GBP kilichopo karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nerere kukifunga maramoja kwa kutofuata maagizo ya Serikali ya kutumia Mashine za EFDs kwenye vituo vya Mafuta. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akizungumza na baadhi ya wakazi wa maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere pamoja na wamiliki wa vyombo vya moto kuhusu umuhimu wa kudai risiti wanaponunua mafuta kwenye vituo vya mafuta, wakati alipokifunga Kituo cha Mafuta cha GBP, baada ya mmiliki wake kubainika kukiuka masharti kwa kutotoa risiti za kielektroniki (EFD)kwa wateja wake. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwa katika mitaa ya maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, akizungumza na baadhi ya wakazi wa maeneo hayo kuhusu umuhimu wa kudai risiti wanaponunua mafuta kwenye vituo vya mafuta na kuitaarifu Serikali wanapobaini wamiliki wa vituo hivyo hawatoi risiti za EFD. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...