Klabu ya Dar es Salaam Gymkhana (DGC) ambayo ni miongoni mwa klabu kongwe za michezo hapa nchini Tanzania, leo imeadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake kwa mtindo wa aina yake uliowakutanisha wadau mbalimbali wa klabu hiyo kupitia chakula cha jioni jijini Dar es Salaam.

Tangu wiki iliyopita, kumekuwa na shughuli mbalimbali za kimichezo ambazo zilianza kufanyika tangu 3 Julai na kilele chake kuwa siku ya leo ya tarehe (08/07/2017). Shughuli hizo ziliandaliwa kwa lengo la kupamba tukio hili muhimu.

Miongoni mwa michezo iliyokuwa ikifanyika ni pamoja na tenisi, kriketi, squash, mashindano ya gofu na michezo mingine mingi.

Mgeni rasmi aliyehudhuria sherehe ya kilele cha maadhimisho hayo wakati wa kufunga michezo hiyo, alikuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ambaye alizungumiza shamrashamra za kuadhimisha miaka 100 ya klabu hii mkongwe.

“Binafsi nimefurahishwa sana kusikia kwamba michezo yote iliyohusishwa kwenye maadhimisho ya tukio hili kubwa na muhimu ambalo imefanyika na kuisha salama kwa kipindi chote cha wiki moja, jambo ambalo linaonyesha waandaaji walijapanga vyema. Ni imani yangu kwamba udhamini wa wadau mbalimbali umewezesha kufanikisha kufanyika michezo yote hii muhimu,” alisema Waziri Dk Mwakyembe.

Dk Mwakyembe alisema matarajio ya serikali ya awamu ya tano ni kuona wadau wanaongeza nguvu kujihusisha zaidi kwenye shughuli za michezo jambo ambalo linaweza kuibua vipaji zaidi kwa Watanzania wote.

Waziri Mwakyembe alimwaga pongezi kwa wanachama wote wa klabu hiyo wa sasa na wale waliopita pamoja na kila mtu ambaye alishiriki kwa nafasi yake kuhakikisha klabu ya Dar Gymkhana inafanikiwa zaidi.

“Ninatambua fikaumuhimu wa klabu hii kwa ngazi ya taifa letu kwani imekuwa miongoni mwa taasisi ambayo imekuwa ikihamasisha kukuza michezo, utalii na kuwakutanisha pamoja watu kwenye matukio ya kijamii,” alisema.

Waziri Mwakyembe aliwataka Watanzania kujenga utamaduni wa kushiriki michezo mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha afya zao na kuwahamasisha wananchi kujiunga na klabu hii ambayo ina michezo mbalimbali. Alisema klabu hii imekuwa ikiwakutanisha wageni kutoka mataifa mbalimbali na Watanzania.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikabidhi kikombe kwa Nahodha wa mpira wa miguu wa Klabu ya Gymkhana Aliabid Mamdani (kulia) baada ya timu yake kuibuka washindi wa jumla katika michuano iliyofanyika hivi karibuni katika kuadhimisha ya miaka 100 ya klabu ya Gymkhana. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jana wakati wa kilele cha maadhimisho hayo jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Mwenyekiti wa klabu ya Gymkhana Walter Chipeta.
Mwenyekiti wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana, Walter Chipeta akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 100 ya Klabu ya Dar es salaam Gymkhana yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam. 
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakeyembe akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 100 ya Klabu ya Dar es salaam Gymkhana yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akisalimiana na Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Dar Gymkhana, George Kritsos wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 100 ya Klabu ya Dar es salaam Gymkhana yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...