Na Shamimu Nyaki-WHUSM

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe amewashukuru viongozi wote wa Serikali, Sekta binafsi, Taasisi za Kidini vyombo vya habari na watanzania wote waliomfariji katika msiba wa mke wake Bibi Linah Mwakyembe uliotokea Julai 15 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa Misa ya mazishi ya mke wake huyo iliyofanyika jana nyumbani kwake Kyela Mhe. Mwakyembe ameeleza kuwa amefarijika sana kwa upendo ulioonyeshwa na kila mtu kwa nafasi yake katika kipindi hiki kigumu na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kila jambo.

“Mimi na wanangu tumefarijika sana kwa kuona jinsi ambavyo Watanzania na wana Kyela mlivvyokuwa na upendo kwetu mmetupa faraja na mmetutia nguvu na mmetuoshesha ushirikiano mkubwa katika jambo hili tunaomba mwenyezi Mungu awabariki sana na asanteni sana”Alisema Mhe Waziri Mwakyembe.

Kwa Upande wake Mhe.Amos Makala Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wakati akitoa salamu za pole kwa niaba ya wanachi wa mkoa wake amesema wananchi wa Mbeya watamkumbuka marehemu  mama Linah Mwakyembe kwa moyo wake wa kujitolea kusaidia jamii katika mambo mbalimbali ikiwemo kufundisha jamii kumcha Mungu pamoja na Ujasiriliamali uliosaidia wanawake wa Kyela kujiajiri.

“Wananchi wa Mbeya tunakupa pole sana Mhe. Mwakyembe pamoja na familia yako lakini pia tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha ya mama Linah hapa duniani ambayo yameleta faida kwa jamii tunamuomba mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi amina lakini na wewe pia tunakuombea Mungu aendelee kukupa uvumilivu na uamini kuwa hili nalo litapita”.Alisema Mhe Makala.

Marehemu Bibi Linah Mwakyembe ameagwa na kuzikwa jana nyumbani kwake Kyela na ameacha watoto watatu.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...