Na Joachim Mushi wa TBN
WAZIRI wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa leo ametembelea mradi wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam na kuridhishwa na kasi ya ujenzi inayoendelea chini ya Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd ya nchini Japan. 
Akizungumza katika ziara hiyo alisema lengo ni kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi huo ili kuhakikisha unakamilika mapema kama ulivyopangwa. Prof. Mbarawa alisema ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo ambao mara baada ya kukamilika utarahisisha shughuli za usafiri kwa wananchi watumiao barabara hizo mbili za Nyerere na Mandela jijini Dar es Salaam. 
Mradi huo wa ujenzi unatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2018 huku ukitarajiwa kugharimu takribani shilingi bilioni 100, ambapo kati ya fedha hizo shilingi bilioni 93.44 zitatolewa na Japan kupitia Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 8.3.   
Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd inayojenga barabara za juu eneo la Tazara, Kiyokazu Tsuji (kulia) akitoa maelekezo kewa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati) maendeleo ya daraja hilo wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya mradi huo. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida akishuhudia. Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd inayojenga barabara za juu eneo la Tazara, Kiyokazu Tsuji (kulia) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati) muonekano wa ramani ya daraja hilo na ujenzi unavyoendelea wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya mradi huo. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida akishuhudia.  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akipata maelezo juu ya maendeleo ya mradi huo Muonekano wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam. Muonekano wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...