Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiana na
watumishi wa kitupo cha afya cha mji mdogo wa Katoro, mkoani Geita.Waziri huyo amefika
katika kituo hicho ili kujionea hali ya
kituo hicho ambacho kinahudumia idadi kubwa ya wakazi wa mji huo pamoja na
jirani zake licha ya kuwa na changamoto ya watumishi pamoja na miundombinu.
Waziri
Ummy akimsalimia mtoto aliyefika kituoni hapo pamoja na mama yake kupata huduma
ya afya,kulia ni Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho Dkt. Peter Janga
Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akimfafanulia jambo mmoja wa wagonjwa waliofika
kupata huduma kwenye kituo cha afya cha Katoro
Waziri
Ummy akitoa maelekezo kwenye matangazo yaliyobandikwa kwenye kuta za kituo
hicho,kushoto ni Mkurugenzi wa HALMASHAURI YA Geita Lawrence Kalabezile.Waziri
huyo amewataka watumishi wa kituo hicho kujituma na kutimiza wajibu wao katika
kuwahudumia wananchi hususan katika kuokoa maisha ya wagonjwa.
Katika
ziara hivyo Waziri Ummy alikagua ujenzi wa jengo la upasuaji wa dharura
unaojengwa kwenye kituo hicho.Waziri wa Afya yupo katika ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Geita (PICHA ZOTE NA WIZARA
YA AFYA)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...