THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO ZANZIBAR AZUNGUMZA NA WAANDISHI KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA IDADI YA WATU DUNIANI

Na Maelezo Zanzibar 
Wakati dunia inaungana kuadhimisha siku ya Idadi ya Watu duniani bado uzazi wa Mpango unaonekana ni changamoto katika baadhi ya maeneo ya Zanzibar.

Hali hiyo hupelekea ongezeko la idadi ya watu lisiloendana na kasi ya ukuaji wa uchumi na upatikanaji wa huduma za jamii katika maeneo mbalimbali nchini.Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Khalid Salum wakati akitoa taarifa yake kwa Vyombo vya habari kuelekea maadhimisho hayo hapo kesho.

Amesema ni vyema jamii kujenga mwamko juu ya umuhimu wa suala la uzazi wa Mpango ili kujenga jamii bora, iliyoimara na chachu katika kuongeza kasi ya maendeleo.

Dkt. Khalid amesisitiza jamii kuendelea kutumia njia za asili za uzazi wa mpango ambazo ni salama kwa afya ya mama na kuhudhuria katika Vituo vya afya kupata taaluma ya matumizi ya njia za kisasa pale inapohitajika.
Ameongeza kuwa suala la uzazi wa Mpango limesisitizwa hata katika Vitabu vya Dini ili kumpa nafasi Mama mzazi kurudisha afya na nguvu anazozitumia wakati wa kubeba mimba na kujifungua.

Kila ifikapo July 11, Zanzibar huungana na nchi zingine duniani kuadhimisha Siku ya Idadi ya Watu duniani ambapo kwa mwaka huu Kauli mbiu ni “Uzazi wa Mpango:Kuwawezesha Watu,kuendeleza Mataifa”
 Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na maadhimisho ya siku ya Idadi ya Watu duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo July,11. Kulia yake ni Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Zanzibar Juma Hassan Reli.
 Baadhi ya wandishi wa habari wakifuatilia mkutano wao na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed hayupo pichani uliofanyika wizarani kwake Mjini Zanzibar.
 Mwandishi wa habari wa Idara ya Habari Maelezo Faki Mjaka akiuliza swali kwa Waziri wa Fedha na Mipango juu ya siku ya Idadi ya Watu duniani katika mkutano uliofanyika Wizarani kwake Vuga.
 Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed akitoa ufafanuzi wa maswali alioulizwa na wandishi wa habari.
Picha na Makame Mshenga.