Na: Veronica Kazimoto

ZOEZI la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaendelea nchi nzima ikiwa ni maandalizi ya utafiti huo unaotarajia kufanyika hivi karibuni.

Akizungumzia zoezi hilo, Meneja wa Takwimu za Jamii na Watu, Sylvia Meku wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema mpaka sasa mikoa kumi na tatu (13) imekamilisha zoezi hilo ambapo ni sawa na silimia 50.

“Zoezi la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaendelea vizuri na mpaka sasa wadadisi wamekamilisha kuorodhesha kaya katika mikoa 13,” amesema Sylvia Meku.

Ameitaja mikoa iliyokamilisha zoezi la uorodheshaji wa kaya kuwa ni pamoja na Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Iringa, Njombe na Morogoro. Mikoa mingine ni Mwanza, Tabora, Katavi, Mbeya, Mara, Kagera na Lindi. Zoezi la Uorodheshaji wa Kaya linafanyika mikoa yote ya Tanzania Bara na linatarajia kumalizika mwishoni mwa mwezi Julai, 2017.

Utafiti kama huu mara ya mwisho ulifanyika Mwaka 2011/12 ambao ulionesha kuwa asilimia 28.2 ya Watanzania wanaishi chini ya mstari wa Umaskini wa mahitaji ya Msingi.

Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 unafanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango na baadhi ya Wadau wa Maendeleo kwa lengo la kupata viashiria vya kupima hali ya umaskini nchini.
Mdadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akihoji taarifa za kaya wakati wa zoezi la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaloendelea kufanyika nchini ikiwa ni maandalizi ya utafiti huo unaotarajia kufanyika hivi karibuni.
Mdadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akihoji taarifa za kaya wakati wa zoezi la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaloendelea kufanyika nchini ikiwa ni maandalizi ya utafiti huo unaotarajia kufanyika hivi karibuni.
Mdadisi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akiwaoneyesha wasimamizi namna alivyojaza taarifa za kaya wakati wa zoezi la kuorodhesha kaya kwa ajili ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 linaloendelea kufanyika nchini ikiwa ni maandalizi ya utafiti huo unaotarajia kufanyika hivi karibuni. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL GHULA).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...