Benny Mwaipaja-WFM, Arusha
MKURUGENZI
Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika
Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, amewataka wanafunzi 45 kutoka
Tanzania, Kenya, Uganda na Ethiopia, wanaosoma katika Chuo Kikuu cha
Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia kilichoko mkoani Arusha, kusoma
kwa bidii na maarifa ili waweze kuzisaidia nchi zao kuinua sekta ya
viwanda kwa njia ya utafiti na ubunifu wa teknolojia mbalimbali
Dkt.
Weggoro ametoa rai hiyo alipotembelea Chuoni hapo ili kuangalia
utekelezaji wa programu ya miaka mitano ya kuboresha masuala ya
rasilimali watu inayofadhiliwa na Benki yake kwa gharama ya zaidi ya
shilingi bilioni 8.2
Alisema
kuwa Benki yake imeamua kuwekeza fedha nyingi katika eneo la Sekta ya
elimu ya juu katika nyanja ya ufundi ili kuwapata vijana wa kutosha
watakaoziba pengo lililopo na kuweka misingi mizuri ya maendeleo ya
baadae hasa katika matumizi ya teknolojia na sayansi.
“Nimefurahi
sana kuona wanafunzi wanasoma na wana ari kubwa na kwamba fedha
tulizozitoa zinatumika vizuri, tunadhani hata baada ya mradi huu
wa miaka 5 kukamilika, Benki itaweza kusaidia zaidi ufadhili wa fedha
na vifaa” Alisema Dkt. Weggoro.
Kaimu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Prof.
Joram Buza, ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB kwa ufadhili
huo, hatua iliyoongeza udahili wa wanafunzi katika chuo hicho.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki
Dkt. Nyamajeje Weggoro akizungumza kuhusu umuhimu wa vijana wenye weledi
wa kitaaluma katika kukuza uchumi, alipokutana na wanafunzi wa Chuo cha
Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha (hawapo pichani)
wanaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB)Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (kulia) akiwa na Mkutano na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha Prof. Joram Buza, alipotembelea chuo hicho kuangalia mradi wa kuwafadhili wanafunzi unaotekelezwa na Benki yake.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Arusha wanaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki Dkt. Nyamajeje Weggoro (hayupo pichani) alipotembelea Chuo hicho, ambapo aliwasisitiza kusoma kwa bidii ili kuhimili ushindani katika soko la ajira.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...