Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya
TPB Plc, Sabasaba Moshingi (katikati) akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya
miezi tisa ya program ya Mwanamke wa Wakati Ujao ya kundi la pili yanayoendeshwa
na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa
kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO) jijini Dar
es Salaam jana. Mafunzo yana lengo la kuwaandaa wafanyakazi wanawake kushika
nafasi za juu za uongozi katika makampuni na bodi za wakurugenzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya ATE, Bi.
Jayne Nyimbo (wa pili kushoto), Mkuu wa Idara ya Sheria ya ATE, Suzan Ndomba
(kushoto) ma Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dk. Aggrey Mlimuka (katikati),
wakifurahi na Mkuu wa Kitengo cha mafunzo na maendeleo wa Acacia Mining, Janeth
Lekashingo katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya ATE, Bi. Jayne
Nyimbo (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzu wa Kampuni ya Statoil Tz, Gunnar Mentzsen huku Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Sanjay Rughani akiangalia wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya program ya Mwanamke wa Wakati Ujao
yanayoendeshwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya
Waajiri Nchini Norway (NHO) jijini Dar es Salaam.
Mhadhiri wa Taasisi ya Uongozi ya Afrika
Mashariki na Kusini (ESAMI),
Prof. Apollonia
Kerenge (kulia), akizungumza na washiriki wa kundi la pili wa mafunzo ya miezi
tisa ya program ya Mwanamke wa Wakati Ujao yanayoendeshwa na Chama cha Waajiri
Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na
Shireikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO) jijini Dar es Salaam jana.
Mafunzo yana lengo la kuwaandaa wafanyakazi wanawake kushika nafasi za juu za uongozi katika
makampuni na bodi za wakurugenzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
TIB Corporate, Frank Mugeta (kulia), akizungumza na washiriki wa mafunzo ya miezi tisa ya program ya
Mwanamke wa Wakati Ujao yanayoendeshwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Shireikisho la Vyama vya
Waajiri Nchini Norway (NHO) jijini Dar es Salaam juzi. Mafunzo yana lengo la
kuwaandaa wafanyakazi wanawake kushika
nafasi za juu za uongozi katika makampuni na bodi za wakurugenzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...