Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala siku ya jana alitembelea Kata ya Kitobo Wilayani Missenyi na  kuzindua  Daraja la Kyankoko lenye sehemu tatu zilizowekewa Kalavati ,mradi uliopewa jina la la Novati Rutegaruka Memorial Bridge ambalo ni jina la muasisi na mwanasiasa mkongwe ambaye aliangaingia eneo hilo katika kipindi cha Uhai wake.
 Muonekano wa Daraja la Kyankoko lililopewa jina la Novati Rutegaruka Memorial Bridge Daraja linalovikutanisha Vijiji vya Msibuka na Kayanga katika Kata ya Kitobo Wilayani Missenyi
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (pichani) akiongea na wananchi wa Kijiji cha Kashasha kata Kitobo  waliohudhuria katika mkutano wake wa hadhara,Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala ameweza kuchangia miradi ya maendeleo inayoendelea katika kata hiyo na pamoja na kuahidi kuzifanyia kazi kero mbalimbali kama Uhaba wa wauguzi katika Zahanati na vituo vya Afya,Utaratibu wa Bima ya Afya kwa Wazee na watu wenye Ulemavu kwa kuwapunguzia changamoto wanazokutana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...