THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

Balozi wa Kuwait nchini akabidhi vifaa tiba kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete

 Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasen Al Najem akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasen Al Najem na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (katikati) akikata utepe wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasen Al Najem na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasen Al Najem (katikati) wakikabidhi kwa watoto wenye matatizo ya moyo zawadi ya madaftari wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na baadhi ya wazazi wenye watoto wenye matatizo ya moyo wakati wa hafla ya kupokea vifaa tiba toka Ubalozi wa Kuwait kwa ajili ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasen Al Najem. Picha na Eliphace Marwa - Maelezo