Mkurugenzi wa Masoko, Utafitii na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC, Tully Mwambapa (wa pili kulia) akikabidhi funguo ya gari mpya aina ya Toyota Land Cruser kwa aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni aliyehamishiwa Makao Makuu ya Jeshi hilo Kitengo cha Mafao na Fidia, SACP Suzan Kaganda (wa nne kushoto) ikiwa ni makabidhiano ya gari la kusaidia doria kwa Kituo cha Polisi Kawe, Jijini Dar es salaam. Gari hilo lenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 70, limetolewa na Benki ya CRDB kwa kituo hicho. Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika mchana wa leo katika Kituo cha Kawe jijini Dar es salaam. Wengine pichani kutoka kulia ni Kamanda wa Polisi wa Kinondoni wa sasa, ACP Murilo Jumanne Murilo, Afisa Mtendaji Kata ya Kawe, Husna Nond, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, OCD Jackson Simba pamoja na Mkuu wa Kituo cha Polisi Kawe, ASP Samson Mwambungu. 
Mkurugenzi wa Masoko, Utafitii na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla ya kukabidhi gari kwa Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, jijini Dar es salaam.
Kamanda wa zamani wa Polisi Mkoa wa Kinondoni aliyehamishiwa Makao Makuu ya Jeshi hilo Kitengo cha Mafao na Fidia, SACP Suzan Kaganda akizungumza katika hafla ya kukabidhi gari kwa Jeshi la Polisi Kituo cha Kawe, jijini Dar es salaam.
Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB PLC, Godwin Semunyu akiongoza hafla hiyo.
Meza kuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...