Moja ya Benki inayokua kwa kasi nchini, Benki ya FINCA Microfinance, leo imetangaza kampeni ya miezi miwili inayofahamika kama 'FikaNaFINCA' Kampeni hii itampa fursa anayefwatilia kurasa za kijamii ya benki hiyo nafasi ya kujishindia tiketi ya kwenda na kurudi bure baada ya kuposti picha ya bahasha ya tiketi yenye nembo ya FIKA NA FINCA na pia kupendwa na watu wengi.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya benki jijini Dar es Salaam, Meneja wa Masoko wa Benki ya Finca Microfinance, Nicholus John alisema kuwa washindi watakuwa na nafasi ya kupata tiketi za usafiri wa anga na barabara ya kwenda na kurudi kutoka mashirika ya usafiri wa anga ya ndani ya Air Tanzania (ATCL) na Auric Air na pia kwa mabasi yanayoenda bara yakiwemo mabasi ya kampuni za Ngorika, New Force na Isamilo.

"FINCA inathamini wateja wake na jamii kwa ujumla, katika kuonyesha hilo, ndo maana tumeleta kampeni hii itakayoenda kwa miezi miwili huku mshindi kutangazwa kila wiki. Jinsi ya kushinda ni rahisi sana, piga picha tiketi yako yenye nembo ya FIKA NA FINCA, posti kwenye kurasa ya Facebook na Instagram ukiweka #FikaNaFINCA kwenye caption, alafu aalike ndugu jamaa na marafiki kuipenda."alisema John.

John aliongeza: "Ninatoa wito kwa Watanzania kuchukua fursa hii ya kipekee na kushiriki kwa wingi ili kushinda ofa hii ya kusafiri bure".

Meneja wa Masoko wa Benki ya Finca Microfinance Bw. Nicholous John, Benki ya FINCA Microfinance Bwana Nicholous John akionyesha mfano wa tiketi ya ndege itakayotumika katika kampeni yao iliyopewa jina la FikaNaFINCA iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Afisa Mawasiliano wa Shirika la ndege la Tanzania ATCL Bi. Lilian Fungamtama

Kutoka kushoto ni Meneja usafirishaji wa kampuni ya Super Feo Bw Masumbuko akifuatiwa na Meneja wa Masoko wa Benki ya Finca Microfinance Bw. Nicholous John, Afisa Mawasiliano wa Shirika la ndege la Tanzania ATCL Bi. Lilian Fungamtama Bi. Lilian Fungamtama na Mtaalamu wa Masoko wa Benki ya FINCA Bw. Noel Mulumba wakionyesha mifano ya tiketi za usafirishaji ambazo wateja watapaswa kupiga picha na kushirikisha  wafuasi wako katika mitandao ya kijamii ili kujishindia tiketi ya bure katika kampeni iliyopewa jina la FikanaFINCA .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...