THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Benki zashauriwa kubuni bidhaa zitakazo wavuta masikini

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Miraji (wa tatu kulia) akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa tawi la NMB Ikungi.

MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu ameyashauri mabenki ikiwemo NMB kubuni bidhaa zitakazowanufaisha Watanzania maskini ili kuondoa dhana inayowabaguzi ya kuwa "‘maskini sio rafiki wa taasisi za kifedha". Mtaturu ametoa wito huo juzi wakati akifungua rasmi Tawi la Benki ya NMB Ikungi. 

Alisema kuendelea kuamini kwamba maskini sio rafiki wa mabenki, kundi hilo la Watanzania litaendelea kudidimia ndani ya lindi la umaskini. “Kaeni muangalie kundi hili la watu maskini litanufaikaje na huduma zinazotolewa na mabenki ikiwemo ninyi NMB. 

Kundi hili la Watanzania maskini ili liweze kujikomboa kiuchumi, basi mabenki badala ya kutoa mikopo ya fedha taslimu, toeni mikopo ya mizinga ya nyuki, mabwawa ya kufungia samaki au kuku kwa ajili ya kufunga kibiashara”, alishauri Mtaturu. 
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi rasmi tawi la NMB Ikungi.

Akisisitiza,mkuu huyo wa wilaya, alisema ili Mtanzania akiwemo maskini aweze kupata maendekeo ya kweli ni lazima ajiongeze kwa kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za kifedha. “NMB ninyi mnakwenda vizuri na mnakwenda na wakati. 

Mmeendelea kubuni bidhaa/huduma mbalimbali ambazo zimepelekea kuvutia Watanzania zaidi ya milioni mbili kufungua akaunti kwenye matawi yenu nchini kote”, alisema na kuongeza; “Sasa mmebuni akaunti ya FANIKIWA, ambayo inawalenga wajasiriamali wadogo wakiwemo baba/mama lishe na wauza chips. Hongereni sana”. Meneja wa NMB kanda ya Kati, Straton Chilongola (wa tano kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni tano vilivyotolewa na NMB.

Mtaturu alisema sasa umefika wakati wa kuliangalia upya kundi la Watanzania maskini,ili na lenyewe liweze kushiriki kikamilifu kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa kati. Aidha, Mtaturu ametumia fursa hiyo kuwaalika wakazi wa wilaya ya Ikungi wahakikishe wananufaika kikamilifu na huduma mbalimbali zinazotolewa na tawi la NMB Ikungi.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI