Wananchi 365 wa kijiji cha Chongoleani watafidiwa
shilingi bilioni 3,035 kwa ajili ya kutoa
maeneo yao, ili kupisha ujenzi wa bomba la mafuta linalojengwa kutoka Hoima
nchini Uganda mpaka Tanga.
Hayo yamesemwa na Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Usimamizi wa Bandari Tanzania TPATanga, Bibi Janeth
Rwuzangi katika mahojiano maalum na Idara ya Habari (MAELEZO) leo.
Bi Ruzangi amesema
kuwa kwa hapa Chongoleani mradi una ukubwa wa hekta 200 zikiwemo hekta 100 zitakazotumiwa kuweka
miundombinu ya mafuta ghafi. Hekta 100 zilizosalia zitatumika kwa ajili ya
shughuli za TPA) kuwekeza miundombinu ya kupokea mafuta yaliyosafishwa. Vile
vile eneo hili limezingatia maendeleo endelevu ya biashara ya mafuta na gesi
katika siku zijazo.
Aliongeza kuwa TPA itakuwa na wajibu wa kuhudumia meli, kuhakikisha
usalama wa bidhaa, vyombo na watu pamoja na kusimamia masuala ya afya
bandarini. Aidha, Majukumu la TPA
yanatarijiwakujikita katika shughuli za uendeshaji wa majini ikiwemo kuwa na
vyombo na boti maalumu kwa ajili ya kuongozea meli wakati wa kuingia na kutoka
kwenye gati la mafuta ghafi.
Akitoa ufafanuzi, Bi Ruzangi amesema vile vile, TPA ina jukumu la
kuhakikisha inahudumia shehena ya vifaa vyote vya ujenzi katika Bandari ya
Tanga kwa kushirikiana na Bandari Kuu ya Dar es Salaam. Shughuli nyingine ni
pamoja na ulinzi wa miundombinu ya majini pamoja na usalama wa eneo la Bandari
ambalo limegawanyika katika sehemu kuu mbili; ardhini kwenye gati la mafuta na
majini kwenye lango la kuingilia meli na nangani.
Kwa upande wa ajira za TPA Ruzangi amesemawafanyakazi ambao
wataajiriwa ni pamoja na mabaharia, wahandisi, mafundi, wahasibu, wachumi,
watakwimu, vibarua mbalimbali kwa ajili ya nguvu kazi n.k. Sehemu ya wafanyakazi
hawa watatokana na waliopo sasa kwenye Bandari watakaopangiwa kazi hizo. Hata
hivyo TPA inatarajia kuajiri wengine ambao watalazimika kufanya kazi hizo
kulingana na taratibu za ajira za TPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...