Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe amekutana na wasanii wa nyimbo za Injili leo Jijini Dar es Salaam kusikiliza changamoto zinazoikabili tasnia ya muziki wa nyimbo za injili na kuweka mikakati ya kuzitatua changamoto hizo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Akizungumza wakati wa mkutano na wanamuziki wa nyimbo za Injili Mhe. Mwakyembe amesema kuwa serikali ina wajibu wa kufuatilia changamoto za tasnia ya muziki ukiwemo muziki wa injili na kuzitatua ili kuweza kukuza kazi za wasanii kwa maslahi ya mtu mmoja mmoja na taifa.

“Muziki ni tasnia ambayo imewabeba vijana wengi hapa nchini, serikali ina wajibu wa kutetea, kulinda na kuhakikisha maslahi ya kazi za sanaa ikiwemo muziki wa injili inaheshimiwa na kulindwa” Amesema Mhe. Mwakyembe

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bibi. Doreen Sinare amewataka Wasanii wa Muziki wa Injili kutoshawishiwa kutoa malipo yoyote katika vyombo vya habari ili nyimbo zao ziweze kuchezwa kwenye vyombo hivyo bali vyombo vya habari ndio vinapaswa viwalipa wasanii wakati wanapotumia nyimbo zoa.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Wasanii wa Nyimbo za Injili (hawapo pichani) wakati wa mkutano na wasanii hao kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam. 
Katibu Mtendaji Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bibi. Doreen Sinare akifafanua jambo wakati wa mkutano na wasanii wa nyimbo za Injili kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMWITA) Bw. Addo Novemba akiwasilisha changamoto zinazokabili muziki wa injili hapa nchini wakati wa mkutano na wasanii wa nyimbo za Injili kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam. 
Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili Bi. Christina Shusho akichangia hoja wakati wa mkutano na wasanii wa nyimbo za Injili kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na viongozi kutoka serikalini pamoja na viongozi wa chama cha Muziki wa Injili Tanzania baada ya mkutano na wasanii hao kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam. Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...