JUMUIYA ya Madola imeahidi kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo kama ilivyo kwa wanachama wengine wote 52 wa Jumiya hiyo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola  Baroness  Patricia Scotland aliyasema hayo leo wakati alipofanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein Ikulu mjini Zanzibar.
Katika maelezo yake Katibu Mkuu huyo alieleza kuwa Jumuiya ya Madola inaendelea kutekeleza mipango na mikakati kabambe ambayo imeiweka kwa wanancha wake ikiwemo Tanzania ambapo Zanzibar pia, ni miongoni mwao.

Baroness  Scotland alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Rais Dk. Shein kwa juhudi kubwa anazozichukua katika kuhakikisha Zanzibar inakuza uchumi na kuimarisha amani na utulivu na kusisitiza kuwa Jumuiya anayoiongoza haitokuwa nyuma kumuunga mkono.
Aidha, Baroness  Scotland alimueleza Dk. Shein miongoni mwa mipango ya Jumuiya hiyo kwa nchi wanachama wake wote 52 ikiwa ni pamoja na kuongeza fursa katika sekta ya biashara nan uchumi, kuwasaidia wanawake, vijana, upatikanaji ajira kwa vijana, elimu, kutunza mazingira, uwezeshaji na mengineyo.
Aliongeza kuwa uchumi kwa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo umekuwa ukiimarika kwa kiasi kikubwa kwa zile nchi za Bara la Afrika na hata nchi za Bara la Asia uchumi wake umeimarika kwa asilimia 5 hadi asilimia 8.
 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Baroness Patricia  Scotland alipofika Ikulu Mjini Unguja leo akiwa katika ziara ya siku moja na ujumbe aliofuatana nao.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Baroness  Patricia  Scotland alipofika Ikulu Mjini Unguja leo akiwa na ujumbe aliofuatana nao katika ziara ya siku moja. 
/Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiagana na mgeni wake mara baada ya kumaliza mazungumza na  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola  Baroness  Patricia  Scotland alipofika Ikulu Mjini Unguja leo. 
Picha na Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...