Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Exim Dinesh Arora [kulia] akitia saini kwenye kitabu cha wageni akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Exim Tanzania Yogesh Manek walipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini China. Pamoja nao ni Balozi anayewakilisha Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki.

Ujumbe wa kiwango cha juu kutoka EXIM Bank Tanzania wametembelea China wakijaribu kuunda ushirikiano na taasisi za kifedha muhimu za nchi hiyo kwa lengo la kuwezesha biashara kwa urahisi kati ya China na Afrika, haswa kwa biashara ndogo na kati (SME) zinazoendeshwa nchini Tanzania, Uganda, Djibouti na Comoros ambako benki ya Exim inafanya biashara.

Mikutano iliyofanyika nchini China ilifanikishwa na Balozi Mbelwa Kairuki ambaye anawakilisha Tanzania nchini humo kwa kuunganisha ujumbe huo na taasisi muhimu za kifedha za China. Ujumbe huo ulifanya mikutano yenye mafanikio makubwa na benki zinazoongoza za biashara na taasisi za fedha za maendeleo (DFIs).

Safari hii ilikuwa ni muhimu haswa ukizingatia uhusiano unaokua wa kiuchumi kati ya Afrika Mashariki hususani nchi za Tanzania, Uganda, Djibouti na China. Nchi hizi zimeshuhudia mwongezeko mkubwa wa uwekezaji na biashara katika miaka ya hivi karibuni kupitia makampuni makubwa ya kiserikali na binafsi ambayo yanafanya biashara katika nchi hizi.

Biashara za kati na ndogo (SMEs) zinatambulika kwa umuhimu wake katika kuchangia ukuaji na maendeleo ya uchumi katika nchi zinazoendelea. Huko China biashara hizi zinachangia hadi asilimia 60 ya mapato ya taifa. Katika Afrika mchango unakuwa mdogo kwa sababu mbali mbali zikiwemo ukosefu wa vifaa, teknolojia na uwekezaji wa kutosha. Ugumu wa kupata fedha au mtaji unaendelea kuwa changamoto kubwa katika ukuaji wa biashara hizi ambapo inasababisha biashara hizi kufa au kupungua.

Afrika kwa ujumla na zaidi hasa Tanzania, ina fursa kubwa katika maeneo kama ngozi, nguo, usindikaji, kilimo na viwanda. Fursa ni kubwa na juhudi za pamoja zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuendeleza hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali na sekta binafsi.Safari kama hii iliyofanyika hivi karibuni ni hatua nzuri katika kufanikisha juhudi hizi.

Mazungumzo yaliyofanyika yalihusisha kuwepo kwa ushirkiano kati ya benk ya Exim na taasisi za kifedha za China katika kuendeleza sekta ya biashara za kati na ndogo nchini Tanzania. Ilidhihirika kuwa benki ya Exim ikiwa kama moja ya benki zinazoongoza nchini Tanzania katika sekta binafsi inaweza kuwa kichocheo na mstari wa mbele katikakufakikisha mipango hii

Mwakilishi wa benki ya Exim wa dawati la China Katusime Nzarombi amesema, “Tulipokelewa vizuri sana na wenyeji wetu kutoka benki za China na uhusiano ulioanzishwa utaendelea kuboresha uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizi mbili. Tutaendelea kufanyia kazi ushirikiano huu na kuhakikisha kuna faida za uhakika katika sekta ya SME nchini Tanzania.”

Benki ya Exim Tanzania ni moja kati ya benki za biashara zinazoongoza ikiwa na matawi katika nchi nne Afrika. Benki hii inaendelea kuwa mstari wa mbele katika utoaji suluhisho kwenye huduma za kibenki kwa watu binafsi, biashara ndogo na makampuni makubwa. Benki ya Exim ina msingi wa mali wenye thamani ya shilingi za Kitanzania trilioni 1.8 na ina matawi 45 na wafanyakazi 942 katika nchi hizo nne.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...