THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

IDARA YA UHAMIAJI:MGOMBEA URAIS WA TFF WALLACE KARIA NI RAIA HALALI WA TANZANIA

Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanga
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Idara ya Uhamiaji Nchini imethibitisha kuwa  Kaimu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wallace John Karia ambaye ni Mgombea Urais wa TFF  katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika August 12  mwaka huu ni Raia halali wa Tanzania.

 Akizungumza na waandishi habari makao makuu ya Idara hiyo, Msemaji Mkuu wa Uhamiaji,  Ally Mtanga amesema kuwa mmoja wa wagombea wa Urais wa TFF alimkatia rufaa mgombea mwenzake Wallace Karia kuwa si raia wa Tanzania  hali ambayo inafanya akose sifa ya kuwa mgombea wa kiti hicho.

 "Wallace Karia ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa chini ya kifungu cha 5(1) na (2) cha sheria ya uraia ya Tanzania sura ya 357(Rejeo la 2002) na kanuni zake, wakati huo huo akiwa raia wa Somalia kwa kurithi".

Mtanga amesisitiza  utambuzi wa uraia upo kisheria sura ya 357 (rejeo la 2002} uraia hauangaliwi Rangi, kabila wala dini.
 Idara hiyo imevitaka vilabu vyote na taasisi za michezo kuhakikisha wafanyakazi wote na wachezaji ambao raia wa kigeni wanatimiza taratibu zote za kisheria za kukaa nchini  bila kufanya hivyo sheria itashika mkondo wake .