Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo amewapongeza viongozi na watendaji wa wilaya na halmashauri ya wilaya ya Rorya kwa mahusiano mazuri waliyonayo katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Jafo alitoa sifa hizo alipokuwa wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi na kuongea na watumishi .

Katika ziara hiyo, Jafo alifanikiwa kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, mabweni, maabara, na vyoo kwa sekondari ya Nyamtinga na Nyamunga ambapo majengo hayo yamebainika kujengwa kwa ubora wa kuridhisha. 

Ujenzi wa miundombinu hiyo imegharimu zaidi ya sh.milioni 500 kutoka serikali kuu kwa lengo la kuboresha elimu hapa nchini
Kwa upande wake,Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara, Agness Marwa amempongeza Naibu Waziri huyo kwa kufika wilayani Rorya na kwamba amekuwa Waziri pekee aliyefanikiwa kutembelea wilayani humo katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano. 


Mbunge huyo ameishukuru serikali kwa upendo wake wa kuisaidia wilaya hiyo miradi ya maendeleo. Naibu Waziri Jafo leo amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku sita ya kukagua miradi ya maendeleo na kuongea na watumishi kwa mkoa wa Kagera na Mara na anaendelea na ziara yake katika mikoa mingine.

.Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikata utepe na kuweka jiwe la msingi katika shule ya sekondari Nyamtinga wilayani Rorya. 
Baadhi ya vyumba vya madarasa vilivyokaguliwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo. 
Mbunge wa Vitimaalum Agnes Marwa akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo. 
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na wananchi wa Rorya na kuwapongeza kwa ujenzi wa madarasa na mabweni. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...