Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka watoa  huduma za afya katika kituo cha afya cha Matei wilayani Kalambo kutoa huduma bora kwa wanawake wajawazito.

Rai hiyo imetolewa jana na Waziri huyo alipokuwa kwenye ziara ya kikazi wilayani hapo na kutembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa sekta ya afya kujua changamoto zinazowakabili. Alisema wajawazito wanapaswa kupata huduma bora kila wanapofika kliniki kila mwezi kwa kuangaliwa mfano dalili za kifafa cha mimba ,wigi wa proteini pamoja na viatarishi vingine  vinavyoweza kusababisha  uzazi pingamizi na hivyo kupelekea vifo kwa mama au mtoto wakatiwa kujifungua.

“Nawapongeza sana kwa kutenga dirisha la wazee ila kusiwepo tu dirisha bali muwape dawa wazee wasio kuwa na uwezo,hivyo kama kuwakatia mfuko wa bima ya jamii (CHF)ni gharama basi wapatieni vitambulisho vya matibabu bure ili wazee wakija kwenye matibabu wasije na barua za watendaji wa vijiji”.

Kwa upande wa madawa Waziri Ummy amewaambia watendaji hao hakuna masharti magumu ya ununuzi wa madawa na vifaa tiba kwa kutumia pesa za CHF“nimeshawaambia MSD ndani ya masaa ishirini na nne umeagiza vitu MSD hana,ndani ya masaa hayo kama hana unaruhusiwa kwenda kununua unapotaka kwenda”hivyo ni vyema wakapitisha wadhaburi watakaokuwa wananunua.

“Tangu serikali hii iingie madarakani imefanya mabadiliko makubwa katika upatikanaji wa dawa kwa kuongezwa bajeti ya dawa kwa asilimia kubwa,hizi changamoto ndogondogo zipo ila mwisho wa siku wananchi wanahitaji dawa,hivyo kuhakikisha dawa zile muhimu zinapatikana wakati wote.

Hata hivyo amewataka kuwapa kipaumbele wale wanaotumia bima ya afya,nataka kuona mnaongeza wananchi watakaotumia bima ya afya kwenye matibabu ili kuweza kutatua changamoto za sekta ya afya.

Upande wa Malaria Waziri Ummy vipimo vya haraka vya malaria vya MRTD ni bure pamoja na dawa ya kutibu Malaria’ALU’ ni bure”asije kuwaambia mtu kipimo hicho utoe pesa,sindano kama mtu amezidiwa na maralia kali ni bure”alisisitiza Waziri Ummy. Akiongelea ugonjwa wa Kifua Kikuu”TB” Waziri huyo alisema ni wakati wa kuwaambiwa watu Tb inatibika kwani katika kila watu mia moja wanaoumwa kifua kikuu na kutumia dawa watu tisini wanapona kabisa na wanaendelea na shughuli zao.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya akina mama waliofika kupata huduma kwenye kituo hicho cha afya.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akimjulia hali mama aliyejifungua kwenye wodi ya wazazi kituoni hapo.
Msafara huo wakiangalia jengo la maabara(halipo pichani) wakati wa ukaguzi wa majengo yaliyopo kituo cha afya Matai Kushoto ni waziri Ummy Mwalimu,katikati ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt.Boniface Kasulu na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Julieth Binyura.
Baadhi ya Watumishi wa Kituo cha afya cha Matai wakimsikiliza Waziri huyo wakati aluipofanya ziara kwenye kituo cha afya kwa ajili ya kujione hali ya utoaji huduma za afya Mkoani Rukwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...