Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Licha ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa amri ya mshtakiwa Harbinder Singh Sethi kutibiwa hospitalini hapa nchini, mpaka leo mshtakiwa huyo bado hajapata huduma yoyote ya matibabu.

 Hayo yamesemwa na wakili wa Utetezi, Alex Balomi, mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shaidi  wakati kesi  hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama mshtakiwa amepatiwa matibabu kama amri ya mahakama ilivyotolewa wiki iliyopita. Alidai, siku mshtakiwa Seth anakamatwa, alikuwa njiani kwenda South Africa kwa matibabu.

Hata hivyo wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Leornad Swai alidai mshtakiwe huuo atibiwe katika Hospitali ya Amana na Lugalo.

Akijibu hoja hiyo, Swai alikiri kuwepo kwa amri ya Mahakama ya mshtakiwa kupatiwa matibabu lakini hakuna ushahidi kuwa siku mshtakiwa alipokamatwa alikuwa anakwenda Afrika Kusini kutibiwa.

Pia alidai suala la mshtakiwa kupelekwa nje ya nchi kutibiwa nje ya nchi bado si sahihi, kwa sababu utaratibu wa mgonjwa kupelekwa nje unafahamika na kwamba haendi kwa sababu ya amri ya Mahakama.

Aliendelea kudai kuwa, madaktari wa hapa  hawajakiri kushindwa na hakuna uthibitisho wa madaktari kwamba wameshindwa kumtibu.

Pia aliongeza kuwa, hakuna utaratibu wa mgonjwa kupelekwa Muhimbili moja kwa moja anatakiwa kuanzia hospitali ya Amana ama Lugalo wao ndio watafanya utaratibu wa kumuhamishia Hospitali ya Muhimbili.

Alidai Magereza ambapo Sethi anatibiwa ndio wanatakiwa kuthibitisha na kufanya utaratibu apelekweHospitali ya Amana.

Alibainisha kuwa Amana nao hawajasema wameshindwa kumtibu hivyo aliomba aendelee kutibiwa katika Hospitali ya Amana.

Kuhusu ombi la Wakili wa Sethi,Alex Balomi kuomba kesi itajwe ndani ya siku saba kwa ajili ya kuangalia kama amepelekwa hospitali, Swai aliomba ipangwe ndani ya Sikh 14.

Alidai kutajwa ndani ya Siku saba ni kumsumbua mgonjwa na kwamba muda huo autumie kwenda hospitali na siyo mahakamani, aliomba ipangwe ndani ya Siku 14 kama utaratibu ulivyo.

Pia alibainisha kuwa ndani ya Siku 14, atakuwa amefikishwa katika hospitali ya Amana ama Lugalo kupatiwa matibabu, utaratibu za Magereza zimekamilika na wao watasimamia.

Hakimu Shaidi katika uamuzi wake alisema hajasema apeleke kutibiwa nje ya nchi, bali atibiwe hapa nchini.

Pia aliwapa siku 14 Takukuru kama walivyoomba awali, ili kuangalia kama atakuwa amefikishwa katika hospitali ya Amana ama Lugalo kupatiwa matibabu.

Kesi imeahirishwa Agosti17,2017.

Katika kesi hiyo, Sethi na James Burchard  Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka  12 ya  uhujumu uchumi  kwa kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kighushi,  kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu,  kutakatisha fedha  na kuisababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...