Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amekutana na wakazi wa Wilaya ya Temeke na Kigamboni katika kusikiliza na kutatua kero za Sekta ya ardhi. Katika mahojiano na wananchi hao, Mhe. Lukuvi amewaonya wananchi kuwa makini na matapeli wanaochukua nyaraka halali za umiliki na kutengeza nyaraka feki.

Hayo yamebainika baada ya baadhi ya wananchi kulalamikia mmliki wa kampuni ya Holland Investment iliyopo  jijini Dar es Salaam kwamba, amekuwa akichukua nyaraka halali za umiliki kwa wananchi kwa lengo la kuwasaidia na baadae kuwabadilishia na kuwarudishia nyaraka feki.
Mmoja wa wananchi kutoka Wilaya ya Temeke (aliyesimama) akieleza kero yake kwa Mhe. Lukuvi wakati wa kusikiliza na kutatua kero za Sekta ya ardhi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akisisitiza jambo kwa wananchi waliofika ofisini kwake kwa ajili ya kutoa kero zao za masuala ya ardhi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...