Baadhi ya Magari ambayo yalitelekezwa katika bandari ya jiji la Dar es Salaam na  baadae yalikutwa na Rais Magufuli kwenye makontena, alipofanya ziara bandarini.

Na Karama Kenyunko blogu ya jamii.
WATUHUMIWA waliongiza magari wakidai ni Nguo wahukumiwa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu wafanyabiashara wawili kulipa faini ya Sh milioni 100 au kufungwa  jela miaka  mitatu baada ya kukiri kuingiza magari matatu nchini na kujifanya kuwa ni mitumba.

 Kitendo hicho  kiliisababishia serikali hasara ya Sh milioni 190.9.
Watuhumiwa hao, ambao ni  Sultan Ibrahim na Ramadhani Hamisi, Raia wa Uganda,  wamehukumiwa adhabu hiyo na Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha.

Akisoma hukumu hiyo, Mkeha amesema, licha ya ushirikiano waliotoa washitakiwa ikiwemo kuomba kutaifishwa kwa magari hayo, ni matakwa ya sheria kwamba mali hizo zitaifishwe na kwamba inazingatia thamani ya magari  hayo ambayo yamevuka kodi iliyotakiwa kupata serikali.

Amesema, kila mshtakiwa anatakiwa kulipa fidia ya milioni 50 au kwenda jela miaka mitatu na magari yote yataifishwe  ili iwe onyo kwa yoyote mwingine mwenye nia ya kukwepa kodi kwa namna hiyo ya washtakiwa.

Kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo, hakimu Mkeha aliuuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusema ambapo, Wakili  wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi ameiomba mahakama kutoa adhabu kwa kuzingatia kifungu namba 203 (b) cha Sheria ya Ushuru wa Forodha ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 ambayo  inataka bidhaa walizokutwa nazo watuhumiwa kutaifishwa.

Hata hivyo, wakili wa utetezi, Jebra Kambore aliiomba mahakama kuwaonea huruma watuhumiwa hao kwani wametoa ushirikiano wa kutosha kwa kuandika barua kwa serikali na kukubali magari hayo kutaifishwa.

Aliongeza, thamani ya magari hayo ni milioni 287,777,536 fedha ambazo ni zaidi ya kodi ambayo serikali ilitakiwa kupata. 

Mapema baada ya watuhumiwa hao kukiri mashtaka, walisomewa Maelezo ya awali ambapo ilidaiwa, Desemba Mosi, 2016 na Machi mwaka huu, washitakiwa hao na wengine wanaoishi Uingereza, walikubaliana kuingiza magari nchini.

Alidai  Oktoba 13, mwaka jana, kupitia nyaraka za kuingiza mizigo bandarini, walishirikiana kuingiza kontena namba 3049836 ambayo ilibeba magari matatu aina ya Range Rover Sports, Range Rover Evock na Range Rover Vogue.
Aidha wanadiwa kutoa taarifa ya uongo kupitia nyaraka hizo za kuingizia mizigo bandarini kwamba kontena hilo lilibeba nguo za mitumba, viatu na magodoro kwa nia ya kukwepa kodi ambayo thamani Mali hizo ilikuwa  ndogo ukilinganisha na thamani halisi ya magari waliyobeba.

Nyantori alidai kutokana na uongo walioufanya, maofisa wa forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) walikadiria kodi ya chini ya S milioni 31.5 badala ya kodi sahihi iliyopaswa kul

Alieleza baadae, ilibainika kuwa kontena hilo lilibeba magari yaliyokuwa yamefichwa ndani ya mitumba ya viatu, magodoro na nguo.

‘’Mshitakiwa Sultan alipekuliwa nyumbani kwake   na kukutwa na funguo tatu za magari hayo.

Awali ilidaiwa, kati ya Desemba Mosi, mwaka jana na Machi 4, mwaka huu, Makao Makuu ya Bandari wilayani Temeke, washitakiwa walitengeneza nyaraka za uongo kuonesha kuwa kontena hilo lilikuwa na mitumba ambayo ni nguo, viatu na magodoro na kuficha ndani yake magari hayo matatu.

Washitakiwa hao pia wanadaiwa kuficha utambuzi wa bidhaa waliyokuwa wakiingiza na kusababisha hasara ya Sh milioni 190.9.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...