Na Lydia Churi-Mahakama

Mahakama ni moja kati ya Mihimili mitatu ya dola wenye jukumu la msingi la kutoa haki sawa kwa wote na kwa wakati. Mhimili huu hufanya kazi ya kutafsiri Sheria mbalimbali zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwapatia wananchi haki. Kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano, Mahakama ya Tanzania imeendelea kusimamia haki za Watoto kama zilivyo haki nyingine wanazostahili kuzipata wananchi wa Tanzania.

UtekelezwajiwahakizaWatoto zilizoainishwakatika mikatabambalimbali yakikandana Kimataifa na kupewa nguvu ya kisheria kupitia Sheria ya Mtoto namba 21yamwaka2009,kunahitajiushirikianobainayaTaasisina wadau wa haki za watoto. Katika kulinda haki za watoto wa Tanzania, hivi karibuni, Mahakama ya Tanzania ilizindua Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) katika jiji la Mbeya na kufanya idadi ya Mahakama hizo kufikia mbili hapa nchini. Mahakama nyingine ya Watoto iko Kisutu jijini Dar es salaam.

Maendeleo Endelevu hupatikana kwakuzingatia misingi ya hakiza Watoto

Kwa kutambua umuhimu wa watoto kuwa ni uhai wa taifa lolote,Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) ilichukua hatua za makusudi kuhakikisha haki za kisheria za watoto zinalindwa kwa kujenga jengo la Mahakama ya Watoto jijini Mbeya. Jengo hili linakuwa ni la pili maalum kujengwa kwa shughuli za Mahakama ya watoto pekee kwa Tanzania bara. 

Akizindua jengo hilo hivi karibuni, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alisema endapo haki za Watoto zitadharauliwa kwa mapanayakesasa,basi azmayamaendeleo endelevu ya nchi hapo baadaye, itakuwa hatarini.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma akikata utepe kuzindua Mahakama ya Watoto (Juvenile Court) leo jijini Mbeya. Hii ni Mahakama ya Pili ya Watoto nchini Tanzania baada ya ile iliyoko Kisutu Jijini Dar es salaam. Mahakama hii imejengwa kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF).

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim JumaakifunguaPaziakuashiriauzinduziwa Mahakamaya Watoto (Juvenile Court) leojijiniMbeya. KatikatiniMwakilishiwa UNICEF nchini, Stephanie ShanlernakushotoniJajiKiongoziwaMahakamaKuuya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali.
Mwakilishiwa UNICEF nchini, Stephanie Shanler akizungumza wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Mahakama hiyo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...