Na Bashir Yakub.

Mwanamke ameachwa na mume wake wa zamani. Lakini hajamuacha kisheria. Hakumpa talaka isipokuwa waliachana tu kila mtu akaendelea na maisha yake tena kwa muda sasa. Wewe umekutana na huyo mwanamke na umeanzisha naye mahusiano. Umeanza kuishi naye au umeamua kabisa kumuoa.

Ulimuuliza kuhusu mahusiano yake ya zamani akakueleza bila kukuficha yaliyomsibu. Na wewe ukaona kwa kuwa tayari hayuko na huyo mume wake wa zamani kwa muda mrefu au muda kiasi basi haina shida. Kitu cha msingi kwako ulichozingatia ni kuwa hawa watu hawako wote tena kwa maana mahusiano yao waliyasitisha.

Je sheria inasemaje kuhusu hali hii. Je kukaa na mwanamke wa namna hiyo kwa maana ya kuishi naye bila ndoa, au kuishi naye kwa ndoa au kuwa naye katika mahusiano bila kuishi naye kumezungumziwaje na sheria. Je uko salama. Je hakuna lolote linaweza kukutokea likakusababishia usumbufu, gharama, na kurehani mustakabali wa maisha yako. Je nini ufanye ikiwa umo katika hali kama hiyo.

Haya na mengine yataelezwa hapa chini. Sura ya 29 ya sheria ya ndoa , iliyorekebishwa mwaka 2010 itatupatia majawabu ya maswali haya.

1.NI WAKATI GANI NDOA HUHESABIKA IMEVUNJIKA.

Ndoa ni zao la sheria na kufa kwake hufa kisheria. Ndoa haivunjiki isipokuwa taratibu za kisheria zimefuatwa. Ndoa inaweza kuvunjika kwa kifo cha mmoja wana ndoa, kwa kupotea kwa mda mrefu na kuihisiwa kufa kwa mmoja wa wanandoa( presumption of death), lakini pia ndoa hufa/huvunjika kwa talaka.

Kama mojawapo ya hayo juu halijajitokeza ndoa hiyo bado inaishi. Kwahiyo mwanaume unatakiwa kujua kuwa mwanamke uliyemuoa au unayeishi nae bila ndoa au uliye naye tu katika mahusiano ya kawaida , ikiwa hapo awali alikuwa katika ndoa na mojawapo ya yaliyotajwa hapa juu hayajatokea basi mwanamke huyo ndoa yake bado inaendelea. Hapo badae itaelezwa hatari kubwa zinazokukabali .

2. JE KUTENGANA NI TALAKA.

Unaweza kudhani kuwa uko salama kwasababu una uhakika mwanamke uliyenaye ametengana na mme wake wa mwanzo na hivyo wewe uko salama. Kisheria kuna tofauti ya kutengana na kuachana/kutalikiana. Kutengana sio talaka. Talaka ni talaka mpaka itolewe kwa mujibu wa sheria. Pia kutelekeza sio kuachana/talaka. Watu wanaokuwa wametengana au wametelekezana bila talaka fahamu kuwa watu hao kisheria bado ni wanandoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Je ni muda gani wanandoa wakitengana,kwa mujibu wa sheri hii itahesabika imevunjika?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...