THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ATEMBELEA BANDA LA NIDA; AFURAHISHWA NA HATUA ZA USAJILI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametembelea banda la Maonyesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA na kufurahishwa na ufanisi mkubwa katika kuunganisha mifumo ya Serikali yenye kulenga utoaji huduma bora na kurahisisha shughuli ya Utambuzi kwa wananchi.
Mheshimiwa Makamu wa Rais ametembelea Banda la NIDA akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kilele cha maonyesho ya sikukuu ya Wakulima Kitaifa maarufu Nanenane yaliyofanyika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi. Mhe. Samia aliambatana na viongozi mbalimbali wa Kitaifa akiwemo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Dr. Charles Tizeba.
Katika maonyesho hayo NIDA ni miongoni mwa Taasisi zilizofanya vizuri na kupata ushindi katika makundi 15 yaliyotangazwa. 
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Banda la maonyesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwenye maonesho ya NaneNane viwanja vya Ngongo mjini Lindi leo. Makamu wa Rais alipokelewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi. Rose Mdami
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea taarifa ya shughuli za Usajili ambazo zimekuwa zikifanyika katika Banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wakati wa Maonyesho ya Nanenane kwenye Viwanja vya Ngongo mjini Lindi.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo toka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi. Rose Mdami
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya mashine zinazotumika kusajili na kutolea vitambuslisho vya Taifa toka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bi. Rose Mdami
Watumishi wa NIDA wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupata ushindi kwenye maonyesho ya Nanenane kwa mwaka 2017.