Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitambulishwa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 37 wa SADC kwenye ukumbi wa OR Tambo mjini Pretoria, Afrika ya Kusini. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Rais wa Zambia Mhe. Edgar Lungu akiwashukuru washiriki wa mkutano huo wakati wa Utambulisho kwenye ufunguzi wa mkutano wa 37 wa SADC kwenye ukumbi wa OR Tambo mjini Pretoria, Afrika ya Kusini.# Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais. 
Mkutano huo wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit),unawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Dkt John Pombe Magufuli.Katika mkutano huo Tanzania itakabidhi nafasi ya Uenyekiti kwa Mwenyekiti mpya.

Double Troika inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji. Katika mkutano huo Mfalme Mswati III wa Swaziland atakuwa ndiye Mwenyekiti. Ajenda kuu katika Mkutano huu ni kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda na hasa nchini DR Congo na Lesotho.
Mwenyekiti wa SADC aliyemaliza muda wake Mfalme Mswati III akimkabidhi Uenyekiti Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika mjini Pretoria, Afrika ya Kusini ambapo Tanzania iliwakilishwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Viongozi wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika mjini Pretoria, Afrika ya Kusini .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

…………………………………………………………………………..

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 19 Agosti 2017, amehudhuria ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika – SADC mjiniPretoria Afrika Kusini akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli.

Mhe. Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa taarifa fupi kuhusu majukumu ya SADC Organ kwa kipindi cha Agosti 2016 – Agosti 2017 kwa niaba ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa SADC Organ anayemaliza muda wake.

Makamu wa Rais amewasilisha kwa Wakuu wa Nchi na Serikali taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya SADC Organ kwa kipindi cha Agosti 2016 hadi Agosti 2017 kwa niaba ya Mwenyekiti wa SADC Organ anayemaliza muda wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Taarifa hiyo inaelezea hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda katika kipindi tajwa hususan katika Nchi za DRC, Madagascar na Lesotho.Aidha taarifa hiyo pia imetoa mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto zinazoendelea kuikabili Kanda katika maeneo ya siasa, ulinzi na usalama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...