THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ATEMBELEA BANDA LA BOT KATIKA MAONESHO YA NANENANE

 Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uhusiano, juu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inafanya kazi katika vitengo mbalilmbali ndani ya maonesho ya Nanene yalifikia kilele jana  katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
  Makamu wa Rais, Samia Suluhu  Hassan  akipokea mfuko wenye taarifa mbalimbali kutoka kwa Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Vicky Msina  katika  maonesho ya Nanene yalifikia kilele jana  katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika  maonesho ya Nanene yalifikia kilele jana  katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
 Waziri wa Kilimo , Mifugo na Uvuvi, Charle’s Tizeba akipata maelezo kutoka Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Bestina Magutu juu Mamlaka hiyo inavyofanya kazi katika  maonesho ya Nanenane yaliyofikia kilele jana  katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
 Afisa wa Mamlaka ya Chakula na Dawa na Meneja wa Kanda ya Kusini (TFDA), Dogratius Ngatunga akitoa maelezo kwa mwananchi aliyetembelea banda la TFDA katika maonesho ya Nanenane mkoani Lindi juu ya madhara ya vipodozi.
 Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu  akipata  maelezo  kutoka kwa  Meneja Masoko wa PBZ, Aisha Mohamed wakati Makamu wa Rais alipotembelea banda  la PBZ  katika maonesho ya Nanenane yaliyofikia kilele jana  katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu  akimpa kikombe cha mshindi wa jumla wa maonesho ya Nanenane mkoani Lindi, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenaerali , Michael Isamuhyo.