Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha Vijijini 
MBUNGE wa jimbo la Kibaha Vijijini, mkoani Pwani  Mhe. Hamoud Jumaa (pichqni) , ametoa msaada wa sh.milioni 2.3 kwa mkazi wa kata ya Janga, Selemani Mgoto (43) ambaye alipata upofu kutokana na kudhurika na vidonge vya malaria vya 'fansidar' mwaka 2012.

Aidha mbunge huyo, amesema ataendelea kumshika mkono Mgoto kwa kumalizia ujenzi wa nyumba anayojenga. Jumaa pia ,anamjengea nyumba kada wa chama cha mapinduzi (CCM) ambaye aliwahi kukitumikia chama zaidi ya miaka 30, mzee Shabani Kifaru (80), mkazi wa kata ya Magindu.


Akizungumza wakati akikabidhi fedha hizo, Jumaa  alisema ataendelea kutatua changamoto za jimbo pamoja na kusaidia makundi maalum. Alieleza, ametoa fedha hizo kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa mtu huyo kuliko chakula ambacho angekula na kuisha.

Alisema licha ya Mgoto kuathirika macho yake lakini anaishi kwenye maisha ya kupanga hivyo nyumba anayojenga itamwezesha kuishi vizuri. Nae Mgoto ,alimshukuru Jumaa kwa msaada aliompatia na kumuomba asichoke kumshika mkono. Hata hivyo, aliwashukuru wadau wengine ambao wameweza kumsaidia tangu apate matatizo yake.
"Mbunge una watu wengi wa kuwasaidia lakini umeniona na mie, naahidi kuzitumia fedha hizi kwa matumizi lengwa ,nilianza ujenzi huu lakini ninekwama kumalizia "alisema Mgoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...