NA HAMZA TEMBA -WMU

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo makani amesema  jukumu la uhifadhi wa Maliasili za taifa sio la Serikali pekee kwakua Maliasili hizo ni urithi wa taifa na kila mwananchi anapaswa  kujua kuwa ana jukumu la kulinda urithi huo kutokana na umuhimu wake kwa taifa na jamii kwa ujumla.

Makani amesema hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mshiri, Jimbo la Vunjo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro katika ziara yake ya siku mbili mkoani humo kwa ajili kuona changamoto za uhifadhi na kutatua migogoro ya ardhi kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.

Alisema askari pekee na mitutu ya bunduki haitoshi kulinda maliasili hizo kutokana na ukubwa wa maeneo yaliyopo ukilinganisha na rasilimali zilizopo. "Maliasili hizi zipo kwa faida ya kila mwananchi, tunawaomba muendelee kuiunga mkono Serikali katika kulinda Maliasili tulizonazo, tunahitaji kufanya uhifadhi shirikishi, utalii uimarike na nchi yetu ipate mapato zaidi tuweze kufikia uchumi wa kati", alisema Makani.

Akitaja miongoni mwa faida hizo, Makani alisema maliasili za misitu husaidia upatikanaji wa mvua, kuweka mazingira bora kwa ajili ya kilimo na upatikanaji wa hewa safi. Kwa upande wa faida za kiuchumi alisema sekta hiyo kupitia utalii inachangia asilimia 17.2 ya pato la taifa na asilimi 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni.

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro, Betrita Loibooki alisema hifadhi hiyo imejenga mahusiano mazuri na wananchi wa vijiji jirani na kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kukabiliana na ujangili ambapo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita hakuna tukio lolote la ujangili wa tembo lililoripotiwa katika hifadhi hiyo.


Niabu Waziri wa Malisili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mshiri wilayani Moshi ,alipotembelea kijiji hicho kusikiliza Changamoto zinazo wakabili hususani katika eneo la Nusu Maili lililopo chini ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...