Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea amevipongeza vikundi saba vilivyoiwezeshwa na Mfuko wa Mbunge kwa kuweza kujiendeleza na kuanza kufikia malengo waliyojiwekea.

Aliyasema hayo katika ziara ya vikundi saba katika kata nne za Wilaya ya Temeke akiwa ameongoza na wawakilishi kutoka Taasisi ya Global Patner ya nchini Uingereza.

Katika kata nne alizotembelea, Mtolea amewaonyesha wageni hao namna wananchi wanavyojikita katika kujiiunua kiuchumi kwa kuunda vikundi vyao binafsi na kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo ufugaji wa kuku wa mayai, kutotoa mayai, upandaji na uuzaji wa miti aina mbalimbali,  na sanaa za mikono kama batiki, vikoba na masuala ya sanaa ya uigizaji.

Mtolea allitembelea kata ya Mtoni, Azimio, Vituka, Makangarawe na Kilakala 
 Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea  akiwa na Meg Munn kutoka taasisi ya Global Patber kutoka Nchini Uingerza na kutembelea kata ya Mtoni katika Kikundi cha Mfendengeni wanaojishughulisha na shughuli za upandaji wa vitalu vya miti ikiwa ni katika mradi unaosimamiwa na ofisi ya Mbunge.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea akiwa na Meg Munn kutoka taasisi ya Global Patber kutoka Nchini Uingerza na kutembelea kata ya Azimio katika kikundi cha Saccos ya Vijana kinachojishughulisha na mradi wa utotoleshaji wa mayai ya kuku.

 Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalla Mtolea akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Serikali ya Mtaa Mtongani Unguja Kata ya Azimio akishuhudiwa na Mweyekiti wa Mtaa huo Zainab Liganja wakati wa ziara ya Mbunge huyo katika Miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika kata saba za Wilaya ya Temeke.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...