THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MWENYEKITI CHARLES MAKOGA : SHERIA MPYA KUTUMIKA KUKUZA MAPATO YA MJI WA MAFINGA


Na fredy Mgunda, Mafinga

Halmashauri ya Mji wa Mafinga mkoni Iringa inatarajia kukuza mapato katika mwaka Mpya wa 2017/2018 kutokana na kuanza kuzitumia sheria mpya za ukusanyaji mapato pamoja na kuvijua vyanzo vingine vya mapato ambavyo ndio vitasababisha kukuza uchumi wa halmashauri hiyo.

Akizungumza wakati wa baraza la madiwani Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga alisema kuwa sheria mpya walizoletewa toka mwezi wa tano zinawapa nafasi ya kuanza kuzitumia wakati wa kukusanya mapato katika maeneo ambayo walikuwa hawakusanyi.

"Tulikuwa hatukusanyi mapato katika maeneo ya stand,sehemu za maegesho ya magari,sokoni na maeneo mengine kwa kuwa sheria zilikuwa bado si rafiki kwetu kwenda kukusanya mapato ila kwa mwaka unaoanza tutakusanya mapato na kukuza mapato kutoka asilimia 56 hadi kuvuka lengo la serikali la asilimia 80" alisema Makoga

Makoga aliwataka wananchi na viongozi kushiriana kukusanya mapato kulingana vyanzo ambavyo madiwani wameviolozesha kwa manufaa ya halmashauri ya Mafinga Mjini ambavyo vipo kisheria kutoka serikali kuu.

Jamani naombeni mchango wetu kufanikisha swala hili la kukusanya mapato ili tufikie lengo la serikali kwa kuwa mwaka huu hatufikia lengo hilo ni aibu kubwa kwa serikali hii ya awamu ya tank ambayo inaenda kwa kasi kubwa kwa kukuza uchumi wa nchi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mafinga Mjini Charles Makoga akizungumza wakati wa baraza la madiwani wa halmashauri hiyo
Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Mji wa Mafinga wakiwa katika baraza pamoja na wataalamu mbalimbali wa halmashauri hiyo.