Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.  Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kushoto) akimsikiliza meneja wa Karakana ya MT. Depot, Mhandisi Julius Humbe alipo kuwa akifafanua jambo, kuhusu taratibu za matengenezo ya magari ya serikali. Mhandisi Masauni alifanya ziara ya siku moja katika karakana hiyo mapema leo, ili kujionea jinsi matengenezo ya magari ya serikali yanavyofanyika.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.  Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akipata maelekezo ya jinsi kifaa cha kieletroniki cha kubaini magonjwa ya magari kinavyofanya kazi kutoka kwa Fundi Yakubu Kibingo wa karakana ya MT. Depot. Kushoto kwa Waziri ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu. Mhandisi Masauni alifanya ziara ya siku moja katika karakana hiyo mapema leo, ili kujionea jinsi matengenezo ya magari ya serikali yanavyofanyika.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.  Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akifafanua jambo kwa watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) alipotembelea karakana ya MT. Depot mapema leo, ili kujionea matengenezo ya magari ya Serikali yanavyofanyika katika karakana hiyo. Kushoto kwa Waziri ni Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu na kulia kwake ni Mkurugenzi wa zalishaji na matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe.
Mafundi wa Karakana ya MT. Depot wakifanya matengenezo kwenye gari, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.  Mhandisi Hamad Masauni, aliyetembelea karakana hiyo mapema leo ili kujionea jinsi magari ya serikali yanavyotengenezwa. Picha na TEMESA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...