Maonyesho ya nane nane yanatakiwa kuweka alama chanya na kuwa na sura ya mabadiliko yanayoonekana kwa macho kwa wakulima na wafugaji wanaoshiriki pamoja na wananchi wanaopata huduma na bidhaa katika maonyesho hayo.

Mgeni rasmi katika Ufunguzi wa maadhimisho ya nanenane kanda ya kati ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Chimbi ametoa rai hiyo mapema jana kwa wakulima, wafugaji na washiriki wakati akifungua rasmi maonyesho hayo huku akiwataka washiriki hao kuitumia fursa hiyo kwa manufaa zaidi.

“Ni vizuri maadhimisho ya Mwaka huu yakaonesha mabadiliko chanya kwa washiriki mliojitokeza katika kuonesha bidhaa zenu mbalimbali na pia kwa wale wote waliofika kwaajili ya kununua au kupata maelezo ya matumizi ya bidhaa hizo, wapate kitu tofauti kitakachooneka katika maisha yao”, amesema.

Dkt Rehema Nchimbi ambaye ametumia muda usipungua dakika 45 kusisitiza umuhimu wa kuwekeza katika kilimo na ufugaji wenye tija ili kuendana na falsafa ya serikali ya awamu ya Tano inayo himiza zaidi Uchumi wa Viwanda.

Aidha ameliomba Jeshi la Magereza na wawekezaji wote wa ndani na nje ya Nchi wafike kuwekeza katika mikoa ya Singida na Dodoma na kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma watahakikisha wanatengeneza mazingira rafiki kwa kila atakayekuwa tayari kuwekeza katika Mikoa hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akitazama bidhaa za mbogamboga katika banda la Wilaya ya Kondoa katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma. 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akisaini kitabu cha wageni katika banda la Mkoa wa Singida katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akipokea zawadi ya kikapu kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dodoma SACP Julius Sang’udi alipotembea banda la jeshi la magereza kujionea bidhaa wanazotengeza katika maonyesho ya nanenane kanda ya kati yanayofanyika katika viwanja vya Nzuguni, Manispaa ya Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...