THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

NBS YAWATAKA WADAU WA TAKWIMU KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZA UTOAJI TAKWIMU


Na Bushiri Matenda Na Agness Moshi - MAELEZO

Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania (NBS) imetoa rai kwa wadau wa Takwimu Nchini kufuata kanuni na taratibu za utoaji takwimu ili kuepusha sintofahamu baina yao, wapokeaji taarifa na Taasisi husika .

Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa wakati akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam leo kufuatia taarifa zisizo sahihi zilizotolewa na Kampuni ya Utafiti ya Geopoll yenye ofisi ya Kanda ya Afrika, mjini Nairobi, Kenya kuhusiana Viwango na Idadi ya watazamaji wa vituo mbali mbali vya habari vinavyorushwa hapa nchini .

“Taarifa zozote zinazohusu utafiti ni lazima zihusishe wadau mbalimbali, na kwa kuzingatia vigezo vyote vinavyotakiwa na mamlaka iliyoidhinishwa kisheria kuhusiana na utoaji takwimu”, Dkt.Chuwa alivitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na uwazi na ukweli, uhusishwaji wa Wadau na kwa kuzingatia weledi.

Aidha, amefafanua kuwa ni vyema Taasisi yoyote inayotaka kukusanya taarifa mbalimbali za takwimu ni budi kushirikisha wahusika ili kuepusha mkanganyiko na upotoshwaji kama ilivyofanywa na Kampuni hiyo kutoka Nairobi, Kenya.

“Takwimu zinazotolewa bila kuzingatia taratibu zinazohitajika hazitatambulika na Serikali kwani utoaji wa Takwimu haufanywi kama unavyohesabu migomba shambani, hivyo ni lazima wahusika wafuate taratibu zote”, alifafanua Dkt.Chuwa.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015. Kwa mujibu wa Sheria hiyo, NBS imepewa mamlaka ya kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji wa Takwimu rasmi kwa ajili ya matumizi ya Serikali na Wadau wa Takwimu.
Mkurugenzi mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Habari maelezo Jijini Dar es Salaam , kushoto Bw. Ephraim Kwisigabo Mkurugenzi Sensa na Takwimu za jamii.