Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, chembe chembe za mkojo wa msanii maarufu wa filamu nchini Wema Sepetu una dawa za kulevya.
Hayo yamesemwa Leo na mkemia kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Elias Mulima (40), ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Wema na wenzake wawili inayosikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba.
Akiongozwa na Wakili wa serikali Constantine Kakula, Mulima amesema, Februari 8 mwaka huu, alipokea sampuli ya mkojo wa Wema ambaye alifikishwa kwenye ofisi hizo akiwa na askari wawili, WP Mary na Inspekta Willy.
Amedai, askari wale walieleza kuwa walifika pale kwa ajili ya kumpima mshtakiwa Wema mkojo, ambapo kabla ya kumfanyia kipimo alimsajili kisha akamakabidhi WP Mary kontena na kumchukua Wema hadi katika choo malumu kilichopo katika ofisi hizo kwa ajili ya zoezi hilo.
"Baada ya kupata chembechembe za mkojo, nilifanya uchunguzi na kugundua kuwa, mkojo wake ulikuwa na chembe chembe za bangi ambapo kitaalamu bangi  inaonekana kwenye mkojo kwa siku 28".
“Bangi inakemikali ambayo inasababisha mtumiaji kuwa na ulevi ambao hauwezi kutibika kirahisi na mtumiaji kuharibika akili” amedai mkemia Mulima.
Aidha  shahidi huyo amesema kabla ya kupokea sampuli ya mkojo, alipokea bahasha kutoka jeshi la polisi iliyopelekwa pale na Detective Koplo Robert ambayo ndani yake alikuta msokoto na vipande viwili vya bangi ambayo vilipelekwa pale kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu.

Amedai baada ya kuvipima vipande vile vilikuwa na uzito wa gramu 1.08  na baada ya kufanyia uchunguzi majani yale yalionyesha kuwa na rangi ya zambarau  ambayo inaashiria kuwa yale majani ya mmea  wa bangi pamoja na msokoto wa bangi. Ameendelea kudai kuwa, aliandika taarifa ya uchunguzi ambayo ilithibitishwa na mkemia mkuu. 
Hata hivyo, shahidi hiyo alipotaka kuwasilisha ripoti hizo kama kielelezo mahakamani wakili wa utetezi, Peter Kibatala alipinga kielelezo hicho kupokelewa na kudai kuwa ripoti haikidhi vigezo vya sheria kwani mshtakiwa yoyote aliyeko chini ya ulinzi kabla ya kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu ni lazima maombi yangepelekwa kwanza mahakamani lakini polisi hawakufanya hivyo.
Naye wakili Constantine alipinga vikali na kudai kuwa, hakuna kifungu kinachosema kuwa ni lazima kupeleka maombi mahakamani kama mshtakiwa atakubali kutii sheria.
Kufuatia mabishano makali, Hakimu Simba ameiahirisha kesi hiyo hadi Agosti 4 itakapokuja kwa ajili ya uamuzi kama kielelezo hicho kipokelewe au la.
 Msanii wa filamu nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, akitoka mahakamani baada ya kesi yake kuahirishwa hadi saa Sita na nusu mchana, ambapo mkemia atakuja kutoa ushahidi wake dhidi ya kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili yeye pamoja na wafanyakazi wake wawili.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...