Video Courtesy of MCL
JUKWAA
la wahariri Tanzania (TEF) limeondoa zuio la kutokutoa habari za Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Mkonda jijini humo leo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Holiday Inn jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga amesema kuwa Mgogoro kati ya Jukwaa la wahariri wa habari na tasnia ya habari na
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam umefika mwisho na kwamba TEF sasa inaruhusu habari zake ziandikwe na mgogoro ule uliokuwepo uwe yaliyopita si ndwele, tugange yajayo"
Tamko hilo la TEF
limekuja baada ya Machi 22 mwaka huu kutoa tamko lao kwa vyombo
vya habari lililokuwa likisema "Zinalaani vikali vitendo vya Mkuu wa
Mkoa katika kuvamia chombo cha habari cha Clouds Media akiwa ameambatana
na Askari wenye silaha.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Theophil Makunga akizungumza na
waandishi wa habari pamoja na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari
jijini Dar es Salaam na kuondoa adhabu aliyopewa Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa
Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge
Mutahaba akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa mkutano wa Jukwaa la wahariri Tanzania
(TEF) na wanahabari. Wa pili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri
Tanzania(TEF), Deodatus Balile na mshisho kulia ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
Katikati ni Makamu
Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania(TEF), Deodatus Balile
akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
leo. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kushoto ni Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba. Habari na picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...