Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa NHIF akipokea cheti cha ushindi Kutoka kwa  Naibu Waziri -Tamisemi Seleman Jaffo wakati wa maonesho ya nanenane Dodoma.
Watendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) wakiwa katika picha ya pamoja.

MFUKO 
wa Taifa wa Bima ya afya(NHIF) umeibuka kidedea miongoni mwa mifuko ya hifadhi  ya jamii iliyoshiriki maonesho ya  kumi ya kilimo na ufugaji inayoendelea Mkoani Dodoma.

Katika maonesho hayo yanayoshirikisha mikoa ya kanda ya kati ya  Dodoma na Singida mfuko wa NHIF ulishika nafasi ya tatu kwa utoaji wa huduma za hifadhi ya jamii.

Akikabidhi vyeti na zawadi kwa washindi mbalimbali waliofanya vizuri katika maonesho hayo Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa (TAMISEMI), Mh.Selemani Jafo amepongeza jitihada za NHIF na mifuko mingine katika juhudi zao za kumkomboa mtanzania katika nyanja mbalimbali.

“Lengo letu ni kuyafanya maonesho haya ya nane nane hapa Dodoma yawe ya kimataifa, hivyo tunatambua mchango wa washiriki wote katika kumsaidia mkulima na mfugaji,” amesema Mh.Jafo

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa NHIF  Anjela Mziray amesema tuzo hiyo ni kichocheo kwa mfuko huo katika kuboresha maisha ya Mtanzania.

Akizungumza mara baada ya kupokea cheti maalumu kutoka kwa Mh.Jafo,Bi Anjela Mziray ameshukuru kamati ya maandalizi ya maonesho hayo kutambua mchango wa mfuko wa NHIF.

“Tuzo hii kwetu ni motisha tosha ,na pia itatukumbusha kuwa tuna deni la kuwahudumia Watanznia tulichokionesha kwenye maonesho hayo ndio majukumu yetu ya kila siku,” amesisitiza Bi.Mziray.

Pamoja na hilo Bi Mziray amewataka wakazi wa Dodoma na maeneo ya jirani kutembelea Ofisi ya NHIF mkoani humo iliyopo jengo la Hazina Ndogo, barabara ya UDOM ili kujipatia huduma zinazotolewa na mfuko huo.

Maonesho ya Nane Nane kanda ya kati yamehairishwa leo lakini  kutokana na maombi ya wadau Mh.Jafo ameongeza siku mbili zaidi ili kutoa fursa zaid kwa wananchi wa kanda ya kati na maeneo jirani kuendelea kupata huduma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...