Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amekutana na Kaimu Balozi wa Marekani Bi. Inmi Patterson ofisini kwake Jijini Arusha.

Katika mazungumzo yao Bi Inmi Patterson amempongeza Mkuu huyo wa mkoa kwa kufanikiwa kuirudisha Arusha katika hali ya amani na utulivu.
“Kwa kweli sisi kama wamarekai tunafurahi sana kuiona Arusha ikiwa katika hali hii kwani Taifa letu ndio linaloongoza kwa kuleta watalii wengi hapa kwenu na sisi kama balozi tuna wajibu wa kuangalia viashiria vyote vya vurugu na machafuko, ila kwa sasa tunawasemea vizuri sana kwa watu wetu, hongera sana Kamishna kwa jitihada zako sasa Arusha ni mahali salama” amesema Kaimu balozi huyo.

Bwana Gambo alimshukuru sana Balozi huyo kwa kumtembelea Ofisini kwake na amemweleza wao kama mkoa wa Arusha wana wajibu wa kukuza Utalii Mkoani humo kwa asilimia kubwa ya mapato ya utalii yanatokana na mkoa wa Arusha.

“Utalii ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu sisi watu Arusha na pato la taifa kwa sekta ya utalii inachangiwa na Arusha kwa zaidi ya asilimia 80% hivyo unaweza kuona namna ambavyo amani na utulivu visipotiliwa mkazo vinaweza kuleta hasara kubwa kwa watu wa Arusha na taifa kwa ujumla wake.” Amesema Mhe Gambo.

Kaimu balozi huyo wa Marekani ameambatana na Bwana Steve Mshauri wa masuala ya Sheria wa Ubalozi huo na Bi. Brinille Eliane Ellis Afisa wa masuala ya Uhusiano wa Ubalozi huo. 
Mhe Gambo akiwa katika mazungumzo na Kaimu balozi wa Marekani Bi Inmi Patterson
Kutoka kushoto ni Afisa Mahusiano wa Ubalozi wa Marekani Bi. Brilliane Ellis, Bwana Steve mshauri wa masuala ya kisheria wa ubalozi huo
Kaimu Balozi wa MArekani Bi Seoung akimkabidhi Mkuu wa Mkoa zawadi ya kitabu chenye historia ya Rais wa Marekani Bwana Barrack Obama. “Ninajua unampenda sana Kiongozi huyu na umekua unamsoma sana, haya ninakupa kitabu kingine kilichoandikwa na New York times” alisema Balozi huyo wakati anamkabidhi Mhe Gambo kitabu hicho.
Mhe Gambo na Kaimu balozi wa Marekani katika picha ya pamoja.
Mkuu wa mkoa wa Arusha akimsindikiza mgeni wake kutoka nje ya ofisi yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...