Na Agness Francis, Globu, ya jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameahidi kutoa msaada wa Miguu ya bandia kwa walemavu wa miguu wasio na uwezo wa kununua Miguu hiyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, Makonda amesema kuwa anatoa fursa hiyo kwa walemavu 200 ambapo itakuwa ni awamu ya kwanza kuweza kufanikisha zoezi hilo.
Makonda amesema zoezi hilo litafanyika kwa awamu kutokana na gharama. Amesema gharama hizo ni changamoto kwa wananchi wake kwa walio makazini na hata wasio makazini na amewaomba watumie fursa hiyo kujitokeza katika zoezi hilo la upimaji vipimo ili kufanikisha leongo
Amesema kuwa zoezi hilo litafanyika kwa siku mbili kuanzia Agosti 14-15 mwaka huu katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa zilizopo Ilala Boma Jijini Dar Es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akionesha Miguu Bandia kwa Waandishi wa Habari wakati kaizungumza nao Ofisini kwake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...