THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

RC PAUL MAKONDA APOKEA VITANDA 150 NA MAGODORO 150 VYENYE THAMANI ZAIDI YA SHILINGI MILION 300

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo amepokea Vitanda 150 na Magodoro 150 vyenye thamani zaidi ya shilingi Milion 300 kutoka kampuni ya mafuta ya Camel chini ya Kampuni tanzu za Amsons Group, iliyoamua kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa katika kuboresha sekta ya Afya.

Akizungumza baada ya kupokea Vitanda hivyo, Makonda amesema amedhamiria kuhakikisha changamoto zote zinazoikabili sekta ya Afya katika Mkoa wa Dar es Salaam zinamalizika ili kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora za afya.

“Sitaacha kutafuta kwa ajili ya Wananchi wa Dar es salaam, nitabisha hodi kila panapostahili ili mradi Wananchi wangu wawe wanapata huduma za Afya katika mazingira mazuri, ili siku moja waone kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli, sisi tunataka Maendeleo na sio Siasa ndio maana hivi vitu vyote tunavyofanya vinatumiwa pia na wapinzani” Alisema Makonda.

Makonda amesema anatamani siku moja kila mama anaekwenda kujifungua alale kitanda kimoja mwenywe na sio kama ilivyo sasa ambapo wanatumia kitanda kimoja kinamama watatu hadi wanne.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa,Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kupokea  Vitanda 150 na Magodoro 150 vyenye thamani zaidi ya shilingi Milion 300 kutoka kwenye  kampuni ya mafuta ya Camel chini ya Kampuni tanzu za Amsons Group iliyomua kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa katika kuboresha sekta ya Afya. 
.Meneja Uendelezaji wa Biashara Kampuni ya Camel Oil,Suleiman Amour (kulia) akimkabidhi   Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa,Paul Makonda Vitanda 150 na Magodoro 150 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Million 300 kutoka kwenye  kampuni ya mafuta ya Camel chini ya Kampuni tanzu za Amsons Group. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.